Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na sasa Chelsea inahaha. Imemchukua Olivier Giroud kutoka Arsenal. Hakuna anachofanya. Imemchukua Gonzalo Higuain kutokea Juventus, lakini bado hayupo katika kiwango cha unyama cha Costa. Namuona akiwa na kilo nyingi kumwezesha kumudu Ligi Kuu ya England.
 
Baada ya kuondoka kwa Didier Drogba, Costa alijitahidi kumudu vema pengo lake. Leo Chelsea inateseka kwa sababu ya kuachana na Costa. Ndani ya uwanja alikuwa mkorofi kama alivyo nje ya uwanja alikuwa mkorofi.
 
Lakini, moja kati ya sifa ya kocha mzuri ni kuweza kuishi na mchezaji mkorofi ndani na nje ya uwanja. Ndio maana Sir Alex Ferguson aliweza kuishi na akina Eric Canton, Paul Ince, Roy Keane kwa nyakati tofauti. Pamoja na ujeuri wake wote lakini Costa anakupa kitu ambacho mshambuliaji anatakiwa kuwa nacho. Jeuri, ana nguvu, mbabe, anafunga. Si ajabu wote waliofuata baada yake walionekana hawafai. Sina uhakika na Higuain.
 
Lakini, hapo hapo kumbuka kuna washambuliaji wachache sana wa daraja la Costa kwa sasa. Ukiwa naye usimuachie. Kuna Costa, Luis Suarez, Roberto Lewandowski, Sergio Aguero, Pierre-Emerick Aubameyang.
 
Sasa hivi Harry Kane ameingia katika daraja hilo. Kati ya washambuliaji hawa hauwezi kumruhusu yeyote aondoke klabuni kwako kisha ukamchukua Morata. Hawa wapo katika daraja lao la peke yao. Katika timu yako unaweza kuachana na Costa ukamleta Suarez au Aguero sio Morata.
 
Kituko kingine cha Conte kilikuwa kuachana na Nemanja Matic na kumchukua Tiemoue Bakayoko. Shetani gani alimpanda Conte? Ndio maana nasaka namba yake ya simu nimuulize kabla sijafa. Haikushangaza kuona Chelsea walipoteza taji msimu uliopita. Msimu huu walau baada ya kuwana Jorginho na Mateo Kovacic wamejaribu kurekebisha safu yao ya kiungo wakiungana na N’Golo Kante vinginevyo Conte angemuachia mzigo mzito Maurizio Sarri. Maamuzi ya Conte nahitaji kuyahoji kabla sijafa.
 
Baada ya kuchukua ubingwa wa England katika msimu wake wa kwanza, Conte alidhani maisha yangekuwa rahisi na angefanya mambo makubwa tena bila mastaa waliompa ubingwa. Haya yalikuwa makosa ya Conte ambayo hapana shaka pia yaligharimu kibarua chake. Kama Higuain akifeli pale kwa Maurizio Sarri, ambaye amemuamini kwa sababu alikuwa naye Napoli zamani bado lawama itabidi zishuke kwa Conte.
 
Kuna wachezaji hawezi kuwaruhusu waondoke kirahisi kwani, inachukua muda kuziba nafasi zao. Ni kama kwa sasa Liverpool wakimuuza Virgil van Dijik. Sawa, unaweza kupata pauni 100 milioni sokoni lakini utampata beki gani kama yeye labda Vincent Kompany, ambaye anaishia hivyo. Hili ndio tatizo la soka kwa sasa. Kuna nafasi ambazo zinazibika lakini zingine hazina mbadala na unahitaji kufanya maamuzi ya kishujaa sokoni.
 
DUNIA ya soka imepigwa na bumbuwazi baada ya staa mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala kupotea katika ndege iliyokuwa inamleta jijini Cardiff kutokea Ufaransa. Sala alikuwa amenunuliwa na Cardiff baada ya klabu hiyo kutoswa na klabu ya Genk katika harakati za kumnunua staa wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta. Ni nani huyu Sala?
 
Mzaliwa wa Argentina

Alizaliwa eneo la Cululu, Santa Fe nchini Argentina mnamo Oktoba 31, 1990 jina lake kamili likiwa Emiliano Raúl Sala Taffarel. Alianza kucheza soka katika klabu ya mtaani kwao San Martín de Progreso mpaka alipotimiza umri wa miaka 15. Baadaye alihamia mji wa San Francisco, Córdoba kukipiga klabu ya Proyecto Crecer. Klabu hiyo ilikuwa ina uhusiano na klabu za RCD Mallorca na Bordeaux ya Ufaransa.
 
Ukwasi wa kufa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…