Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wababe hao wa Ligi Kuu England msimu huu watacheza pambano la mwisho wa msimu dhidi ya Wolves Mei 12 pale nyumbani kwao Anfield na tayari tiketi za mechi hiyo zipo katika ulanguzi wa hali ya juu.
 
Mtandao mmoja wenye makazi yake jijini Madrid ujulikanao kama livefootballtickets.com, ambao umekuwa ukifanya kazi ya uuzaji tiketi tangu mwaka 2004, umetoa ofa ya tiketi kwa watu wawili kwa dau la Pauni 11,900 ingawa tiketi hizo mbili hazihusishi huduma za vinywaji au chakula.
 
Mtandao mwingine wa Hispania, tickets4football.com – ambao ni mtandao mkubwa zaidi kwa mauzo ya tiketi ya timu kubwa za England nao ulikuwa unatangaza tiketi za mechi hiyo ya mwisho ya Liverpool kufikia Pauni 4,044 kwa wapenzi wawili.
 
Mechi mbili kabla ya pambano hilo Liverpool itacheza na Chelsea katika uwanja wao wa Anfield kisha watasafiri kwenda ugenini kucheza na Huddersfield. Mechi za tiketi hizo nazo zimekwenda juu huku mashabiki wakitazamia huenda wakatangazwa ubingwa katika mechi hizo.
 
Liverpool haina nguvu yoyote ya kuzuia ulanguzi huo wa tiketi za mechi zao lakini wanaweza kuchukua hatua za kisheria kama wakiwakamata mashabiki ambao wamenunua tiketi za msimu kwa ulanguzi.
 
Mtu mmoja mtaalamu wa masuala ya ulanguzi wa tiketi alisema: “Liverpool dhidi ya Wolves ni tiketi kubwa katika soka kwa sababu mashabiki wanataka kuwa pale, sana sana kama itakuwa siku ambayo Liverpool itatangaza ubingwa. Mashabiki kutoka nje ya Liverpool wapo tayari kulipa chochote kuwa uwanjani kuona historia ikiwekwa.
 
Ni wazi kwamba ni bahati nasibu kwa mashabiki. Inawezekana hata Liverpool isiwe inakaribia ubingwa Mei. Kama wakiteleza watu watakuwa wametumia pesa nyingi bila ya sababu. Lakini hivyo ndivyo mchezo ulivyo. Watu wanatumia pesa sasa kwa sababu kama Liverpool ikiendelea hivi nadhani tiketi zitakuwa ghali zaidi pengine kuliko ilivyo sasa,” alisema mtoa habari huyo.
 
Mpaka sasa Liverpool inaongoza kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya wapinzani wao wa karibu Manchester City ambao mechi yao ya mwisho inatazamiwa kuwa dhidi ya Brighton ugenini na kabla ya hapo watakuwa nyumbani wakicheza na Leicester City katika Dimba la Etihad.
 
Kuna uwezekano mkubwa mbio za ubingwa zinaenda mpaka mwisho wa msimu tofauti na misimu mingine ambapo mabingwa walijulikana wiki mbili au tatu kabla ya kumalizika kwa Ligi hiyo.

Msimu uliopita ubingwa ulichkuliwa na Machester City ambayo iliweka historia ya kufikisha pointi 100.
 
Kuna uwezekano mkubwa mbio za ubingwa zinaenda mpaka mwisho wa msimu tofauti na misimu mingine ambapo mabingwa walijulikana wiki mbili au tatu kabla ya kumalizika kwa Ligi hiyo.

Msimu uliopita ubingwa ulichkuliwa na Machester City ambayo iliweka historia ya kufikisha pointi 100.
 
Back
Top Bottom