Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Herrera alisema ujio wa kocha Ole Gunnar Solskjaer umebadilisha mambo mengi kwenye timu hiyo ikiwamo yeye mwenyewe kuruhusiwa kwenda mbele kushambulia, huku kazi ya kukaba ikiwa ya timu nzima tofauti na ilivyokuwa kwenye kipindi cha kocha Jose Mourinho.
 
Solskjaer amechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya Old Trafford baada ya Mourinho kufutwa kazi mwishoni mwa mwaka jana na tangu Mreno huyo achukue mikoba, Man United imeshinda mechi zote nane alizowaongoza.
 
Baada ya Ijumaa iliyopita kuichapa Arsenal 3-1 na kuwatupa nje kwenye michuano ya Kombe la FA, Herrera alisema: “Tunacheza kwa uhuru sasa hivi, hatubanwi. Hicho ndicho kitu anachotaka Ole tangu alipokuja hapa. Sasa tunafurahia kufunga mabao na timu tunakaba wote.
 
Unaweza kuona kama tunakuwa huru kwenye kucheza na kila mtu akiwa na tabasamu usoni, matokeo yanakuja tu yenyewe. Tunafanya vizuri na siku zote ushindi ni mtamu. Tukikaba tunakaba wote na Ole anataka viungo twende mbele kushambulia ili kuwapa wepesi washambuliaji wetu.
 
Sasa naweza kukimbia kuingia ndani ya boksi la wapinzani. Paul Pogba anaruhusiwa kwenda kushambulia, Ashley Young, Luke Shaw wote wanaruhusiwa kushambulia, hata Nemanja Matic anaruhusiwa kupiga mashuti."
 

Usijiwekee mipaka ya umri bana. Kazamie hata meli hapo bandarini kama unaogopa ndege! [emoji1][emoji1][emoji112][emoji124][emoji124]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…