Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usiku wa leo Jumanne kutachimbika kwenye ile vita ya Top Four na ubingwa, kabla ya shughuli nyingine pevu kushuhudiwa kesho Jumatano. Si unajua tena pale juu kuna mbanano wa pointi? Basi Man United wao itawasikilizia tu Arsenal ikishindwa tu kupata ushindi dhidi ya Cardiff City, basi watajibeba.
 
449008306_207261~2.jpeg
 
Kwenye mbio hizo, United watakuwa nyumbani kucheza na Burnley huku Arsenal ikikipiga na Cardiff, lakini ukweli wa mchezo huo ni kwamba vijana wa Unai Emery wana sharti moja tu kwenye mechi hiyo kushinda, haitakiwi sare, wala kupoteza. Hii ni kwa sababu matokeo hayo, yatawafanywa washushwe hadi kwenye nafasi ya sita kama United itaendeleza moto wao wa kugawa dozi itakapoikaribisha Burnley uwanjani Old Trafford. Gari la Man United kwa sasa limewaka.
 
Matokeo ya timu hizo mbili Man United na Arsenal yataangaliwa sana na Chelsea na Tottenham Hotspur, ambao wao shughuli yao itakuwa kesho. Chelsea na staa wao mpya Gonzalo Higuaín watakuwa ugenini kwa Bournemouth na huku wanapaswa kushinda ili kuendeleza pointi la pointi lililopo kwenye kwenye nafasi ya nne, wakishindwa kufanya hivyo, basi nao itakula kwao.
 
Spurs imetoka kufungwa kwenye mechi iliyopita, walipochapwa na Crystal Palace kwenye Kombe la FA, hivyo itahitaji kushinda mechi hiyo ili kuwa na matumaini ya kufukuzia ubingwa kama si kushika nafasi za juu zinazotoa tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
 
Kwenye vita ya ubingwa, Manr City inatazamiwa kupunguza pengo la pointi kileleni watakapokwenda kuwafuata wagumu Newcastle United. Kikosi hicho cha Pep Guardiola kinachotegemea huduma ya mshambuliaji wake, Sergio Aguero, wakishinda tu basi watakuwa wamebakiza pointi moja kuikamata Liverpool, ambayo itasubiri kesho kukabiliana na Leicester City ya Jamie Vardy. Lakini, naambiwa hivi, mastaa kama Paul Pogba, Pierre-Emerick Aubameyang, Mohamed Salah, Higuain na Aguero ndio watakaoamua mchakamchaka huo kwenye Ligi Kuu England kwamba nani achinjwa na nani atachinjwa.
 
.STAA wa Ufaransa mwenye medali ya ubingwa wa Kombe la Dunia, Bixente Lizarazu amesema Paris Saint-Germain watateseka sana watakapowavaa Manchester United bila kuwepo huduma ya Neymar na kwamba alipaswa kuwapo kwenye mechi hiyo.
 
Lakini, straika wa Man United, Romelu Lukaku ameibuka na kusema wachezaji wote wa wababe hao wa huko Old Trafford wanasikitika Neymar kuwa majeruhi kwa sababu walimtaka awepo uwanjani.
 
Lukaku hataki zile kelele za mashabiki watakaokuja kudai kwamba bahati yetu Neymar hakuwapo wakati Man United itakaposhusha kipigo kwa mabingwa hao wa Ufaransa. Neymar hatacheza mechi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Man United watakapokabiliana na PSG.
 
Lizarazu alisema: “Neymar hayupo dhidi ya Manchester? Hii ni shida. Hakika ni mchezaji anayewanyima usingizi mabeki wa timu pinzani. Kukosekana kwake ni janga kwa PSG.” Lakini, Lukaku amekuwa na mtazamo tofauti na kudai mastaa wa Man United walipenda Neymar acheze mechi hiyo.
 
ARSENAL watashuka uwanjani kumenyana na Swansea City kwenye Ligi Kuu England uwanjani Emirates. Hakika hiyo ni mechi ambayo, Arsenal wanapaswa kushinda ili kuwakimbia Manchester United wanaowakimbiza kwenye mchakamchaka wa kuwania kutinga kwenye Top Four.
 
Lakini, ugumu unakuja pale inapofahamika kwamba Swansea City ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa zikipata matokeo mazuri inapokwenda kucheza dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates.
 
Back
Top Bottom