5.Swansea- mara 3, mechi 8
Swansea City wanaenjoi sana wanapokwenda kucheza Emirates kwenye mechi zao za Ligi Kuu England. Wababe hao wa Wales kabla ya kushuka daraja wakati huo na kisha kurudi tena Ligi Kuu England, walikuwa na straika wao matata kabisa, Michu, ambaye alikuwa moto kwenye kuwatesa Arsenal kwa kuwafunga nyumbani na ugenini. Swansea ni moja ya timu ambazo zimekuwa zikiitesa sana Arsenal inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani. Katika mechi nane, Swansea City iliyokwenda kumenyana na Arsenal kwenye uwanja huo wa Emirates, imeshinda mara tatu. Aston Villa nao wameshinda mara tatu uwanjani Emirates katika mechi 11.