Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini ameridhia makubaliano binafsi mkataba wa kibinasi na klabu ya Shandong Luneng kwa lengo la kuhamia klabu hiyo ya China.
United wamekataa kutoa tamko lolote ikiwa malipo yoyote yamefikiwa kumnunua mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye alitia saini nao mwaka 2018.
Fellaini, 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kima cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.
 
Mwisho wa dirisha la uhamisho wa wachezaji katika ligi ya China ni Februari 28.
Fellaini alitia saini kandarasi mpya ya miaka miwili Old Trafford mwezi Juni mwaka jana lakini hajawahi kukubalika na mashabiki wa United licha ya kukonga nyo za mameneja David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho.
 
Ole Gunnar Solskjaer ametamba na kutetea uteuzi wa kikosi chake kilichoanza dhidi ya Burnley juzi Jumanne na kuwaambia wapinzani wake Manchester United imejibu maswali yote kuhusu ubora wake wa ndani ya uwanja kwa siku za karibuni.
 
Katika mechi hiyo, Man United ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 87 kabla ya kuchomoa mabao hayo yote na mechi kumalizika kwa sare ya 2-2, ikimfanya Kocha Solskjaer kunusurika kupata kipigo cha kwanza kwenye timu hiyo tangu alipochukua mikoba.
 
Solskjaer ambaye ameshinda mechi nane kati ya tisa alizoiongoza Man United tangu alipotajwa kuwa kocha wa muda, alipata sare hiyo dhidi ya Burnley baada ya mabao ya dakika za mwisho kabisa yaliyofungwa na Paul Pogba kwa penalti na beki Victor Lindelof, aliyefunga kwenye dakika za majeruhi.
 
Solskjaer amepata somo kubwa zaidi kwenye mechi hiyo ya sare kwa kile walichokionyesha wachezaji wake kupambana pengine kuliko mechi zote nane alizoshinda ukiwamo ushindi wake dhidi ya Tottenham Hotspur na Arsenal.
 
Wazi tu, nimefurahi kwa staili tuliyopata pointi hii, lakini tungeweza kufunga bao la tatu kwa sababu tu muda ulishaisha. Tulichelewa kuanza ule moto. Nimefurahi walichofanya wachezaji wangu."
 
Baada ya mechi hiyo, Man United ina vigogo kibao kwenye ratiba yake kutoka sasa, ambapo kwanza itamenyana na Leicester City na Fulham na baada ya hapo ni vyuma tu, PSG, Chelsea na Liverpool, mechi tatu zinazoongozana kabla ya kucheza na Crystal Palace na Southampton kisha kuja PSG tena, Arsenal tena na Manchester City.
 
Back
Top Bottom