Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tangu aondoke Jose Mourinho, mambo ni tofauti, kumekuwa na mtazamo chanya zaidi na watu wamekuwa na furaha kubwa, wakitasababu kila wakati. Hilo linasaidia sana," alisema Lukaku.
"Pogba? Kwa sasa anafuraha. Mazoezini amekuwa akiambiwa kila wakati kwamba, anapofurahi basi hata timu inashinda. Baada ya hapo wote tunacheka na kiwango cha kila mchezaji kimekuwa juu.
 
Paul, Marcus, mimi mwenyewe, Anthony, kila mtu yupo tayari kwa kupambana na kila mchezaji anajaribu kumwonyesha kocha kwamba yupo tayari wakati wote.
"Tunavyofanya huko mazoezini inatufanya kila mchezaji aamini kwamba yeye ndiye atakayecheza, kwa sababu ubora wa kila mtu upo juu. Lakini, zaidi ya yote kitu kinachosimama mbele ni timu."
 
Inasemekana kwamba Sarri amelazimika kumtumia meseji tajiri huyo wa Kirusi kufafanua jinsi fomu ya timu hiyo ilivyopotea baada ya kuchapwa mechi mbili za ugenini mfululizo dhidi ya Arsenal na Bournemouth Jumatano iliyopita.
 
Kuna uwezekano mkubwa Abramovich akamfukuza Sarri mwishoni mwa msimu kama Chelsea itashindwa kuingia katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao wakati huu Arsenal na Manchester United zikiinyemelea kwa kasi nafasi hiyo huku Chelsea wakiwa hawana mwendelezo wa ubora.
 
Hata hivyo, Abramovich anatazamiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy ambaye anajulikana kwa tabia yake ya kubania watu wake wasiende kwingine kiurahisi. Abramovich anaweza kulazimika kutoa kitita cha pauni 50 milioni kwenda juu kama fidia kwa sababu kocha huyu Muargentina amesaini mkataba mpya wa miaka minne Mei mwaka jana.
 
Solskjaer alishinda mechi zake nane za mwanzo na akatoa sare katika pambano lake la tisa dhidi ya Burnley ambapo walikamatwa kwa sare ya 2-2 Old Trafford. Hata hivyo vichapo vyake alivyotoa dhidi ya Arsenal katika michuano ya FA na dhidi ya Tottenham katika Ligi vimeanza kuwafikirisha upya mabosi wa timu hiyo na huenda wakampa kibarua cha kudumu.
 
Awali Pochettino ilidaiwa kwamba alikuwa anaitaka kazi hiyo ngumu Old Trafford lakini kwa sasa amejikita zaidi katika kuwania ubingwa na na kikosi chake baada ya kutolewa katika michuano ya FA pamoja na kombe la Ligi.
 
Pochettino ambaye ni kocha wa zamani wa Espanyol na Southampton anapewa sifa kwa kutengeneza kikosi cha ushindani zaidi Spurs licha ya kutopewa pesa za kutosha kununua wachezaji mastaa. Kocha huyo amepitisha madirisha mawili bila ya kununua mchezaji yoyote lakini mpaka sasa Spurs imeachwa pointi nne tu na viongozi wa Ligi Kuu ya England Liverpool.
 
Kwa misimu miwili iliyopita Spurs wamejikita katika Top Four na hilo limeongeza soko kwa Pochettino ambaye pia amekuwa akihusishwa na Real Madrid ambayo mpaka sasa kama ilivyo kwa Manchester United nayo inamtumia kocha wa muda, Santiago Solari baada ya kufukuzwa kwa Julen Lopetugai mwanzoni mwa msimu huu baada ya timu hiyo kuandamwa na matokeo mabovu.
 
50642797_381619012396426_5321906138613741154_n.jpg
 
Back
Top Bottom