Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wenger amekuwa na urafiki wa karibu sana na rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi na jambo hilo limedaiwa linamfanya kocha huyo wa zamani wa Arsenal kufikiriwa kwenda kupewa kazi ya ukurugenzi wa michezo kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Paris. Lakini, Tapie anaamini kumpa ajira mtu mwenye sifa na hadhi kubwa kwenye mchezo wa soka kama Wenger kutaondoa uwezo wa kujiamini wa kocha Thomas Tuchel kwa sababu atakuwa yupo chini ya supastaa wa soka.
 
Wenger amekuwa na urafiki wa karibu sana na rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi na jambo hilo limedaiwa linamfanya kocha huyo wa zamani wa Arsenal kufikiriwa kwenda kupewa kazi ya ukurugenzi wa michezo kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Paris. Lakini, Tapie anaamini kumpa ajira mtu mwenye sifa na hadhi kubwa kwenye mchezo wa soka kama Wenger kutaondoa uwezo wa kujiamini wa kocha Thomas Tuchel kwa sababu atakuwa yupo chini ya supastaa wa soka.
 
Hatawasaidia kitu kabisa. Kocha wao wa sasa ni mzuri. Kama wanadhani mkurugenzi hawaelewani, basi waajiri mwingine, lakini asiwe staa. Katika klabu, watu mnapaswa kuwa makini katika kuajiri watu mastaa kwenye nafasi kama hiyo muhimu.”
 
MAURICIO Pochettino, David Beckham na Zinedine Zidane wamezidi kuibua utata baada ya watu hao watatu kuonekana wakienda kupata chakula cha usiku kwenye mgahawa mmoja huko London kabla ya kuondoka mmojammoja wakipitia mlango wauani.
 
Zidane alikuwa wa kwanza kuondoka akipitia mlango wa jikoni na kutokea uwani, kisha akafuatia Beckham na baadaye Pochettino huku wakiwa wametofautiana kwa dakika tatu tu. Jambo hilo limezua utata mkubwa juu ya watu hao watatu.
 
Lakini, Pochettino anasakwa pia na Real Madrid, mahali ambako Beckham na Zidane waliwahi kucheza pamoja kabla ya mmoja kuwa kocha huko na kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita. Kwenye mgahawa huo waliokwenda ni kwa rafiki yake Beckham, Dave Gardner.
 
Pochettino aliandamana na kocha wake msaidizi, Jesus Perez na jambo hilo ndilo lililoibua zaidi utata. Beckham na Zidane, walikuwa wakicheza pamoja kwenye ile Galacticos huko Bernabeu, wamekuwa marafiki wazuri hadi sasa na wamekuwa na uhusiano mzuri na rais wa Los Blancos, Florentino Perez.
 
Shida inakuja sehemu moja tu, Real Madrid bado wanamtaka Neymar, ambaye anaweza kuwagharimu Pauni 200 milioni kutoka Paris Saint-Germain. Mbrazili, Neymar kwa sasa ameripotiwa kuwa na mpango wa kurudi tena kwenye La Liga na safari hii huenda akatua Bernabeu.
 
KATIKA ardhi ya Liverpool, Manchester City juzi Jumatano imeukwaa uongozi wa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho Desemba katikati mwaka jana na Kocha, Pep Guardiola ameanza kutamba.
 
Mabao mawili ya Aymeric Laporte na Gabriel Jesus yalitosha kuipa City ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton na sasa City inaongoza kwa tofauti ya mabao dhidi ya Liverpool huku wote wakiwa na pointi 62 kileleni mwa msimamo wa ligi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…