Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Una undugu na Damushin ??

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
ni mtu mmoja nakumbuka kama niliwahi kukujibu labda itakuwa umesahau GT, utakapomuoana huyu ni sawa sawa na kumuona Damushin.

naomba unisaidie sababu ipi inayopelekea kuwepo kwa urahisi wa kugundua maandishi ya mtu fulani?
---------->> ni maarifa yetu ya kung'amua matatizo kwa haraka au ni mazoea?

  • damushin = computer
  • roy kim = simu ya mkononi
 
Ni msaidie kujibu. Ni mazoea hasa kwa wewe haubadiliki kiuandishi kabisaaa,ukiwa roy bado kikorea unacho,man u unayo hata wale uliowazoea kwenye damushin na kwenye roy bado unao na unachat nao vile vile unavyochat nao kama damushin
 
ED Woodward, katika ofisi moja ya mabosi zake, pale New York Marekani au Dubai, au popote duniani, atakuwa anatazamana na mabosi wake matajiri familia ya Grazer Mei mwaka huu kujadili habari nzito. Nani awe kocha ajaye wa Manchester United?
 
Kwa sasa jibu linaweza kuwa rahisi. Ole Gunnar Solskjaer. Jibu rahisi sana kwa sasa. Ametoka sare moja tu katika mechi zote alizoisimamia timu hiyo tangu aichukue kwa Jose Mourinho siku chache kabla dunia haijala pilau ya Krismasi mwaka jana.
 
Mabosi wake watakuja sura. Kwanini Ole Gunnar? Jibu lake litakuwa jinsi ambavyo aliibadili timu baada ya kuikuta hoi katika mikono ya Jose Mourinho. alikuta hakuna matokeo uwanjani. Nje ya uwanja alikuta Jose haongei na Paul Pogba, haongei na Luke Shaw vema, haongei na Anthony Martial vema, haongei na wachezaji wengi vema.
 
Sasa hivi yeye anaongea nao vema. Sasa hivi chini yake timu yake inashinda. Inaweza kuwa sababu ya kumpa timu. kwa mtazamo wangu hapana. Timu ambayo inatoka kwa kocha mkorofi kwenda kwa kocha mwingine ina nafasi ya kupata matokeo mazuri.
 
Ikifika msimu ujao, maisha yaanza upya. Binadamu wanarudi katika ubinadamu wao. Ile morali inaweza kuyeyuka kwa sababu watu wanaanza kuzoea mabadiliko. Mazoea yanarudi. Hapa ndipo Solskjaer anapoweza kujikuta katika wakati mgumu.
 
Iliwatokea Chelsea. Machi 2012 walipomfukuza Mreno mwingine, Anre Villas-Boas walimchagua Roberto Di Matteo kuwa kocha wao wa muda. Ghafla akabadili kila kitu. Wakachukua FA na kisha wakachukua ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yao na historia ya timu za London.
 
mwishoni mwa msimu walimchagua kuwa kocha wa kudumu. Alidumu kwa miezi minne tu. alifukuzwa Novemba 2012. Kisa? Matokeo mabovu. Kwanini? Inaweza kuwa wachezaji walipandisha morali alipoingia yeye, halafu katika msimu uliofuata wakarudi katika mazoea ya kawaida.
 
Hiki ndicho ambacho kinaweza kumtokea Solskjaer? Nadhani matajiri wa United pamoja na watu wengine wa bodi wanaweza kumpa Woodward kuhusu mfano huu wa Di Matteo. Sijui atawaambia nini. Inawezekana ndio maana kuna watu ndani ya United bado wanataka Mauricio Pochettino wa Tottenham apewe kiti hicho bila ya kujali kile ambacho Solskjaer anakifanya kwa sasa.
 
Huu ni msimu wa tatu mfululizo Spurs inawania ubingwa huku ikiwa imetulia Top Four na safari hii wamefanya hivi bila ya kutumia pesa yoyote katika madirisha mawili ya uhamisho yaliyopita. Hawakununua mchezaji katika dirisha kubwa la mwaka jana na wala hawakununua mchezaji katika dirisha la Januari. Sana sana wamemruhusu Moussa Dembele kwenda China.
 
Tatizo ni moja, Pochettino hajawahi kutwaa taji lolote kama kocha katika maisha ya kazi hiyo. Akiwa na Espanyol, Southampton na kisha sasa hivi pale Spurs hajawahi kutwaa taji lolote. Ana mbinu za kushinda mataji au kuiimarisha timu tu? hili ndio swali.
 
Tatizo ni moja, Pochettino hajawahi kutwaa taji lolote kama kocha katika maisha ya kazi hiyo. Akiwa na Espanyol, Southampton na kisha sasa hivi pale Spurs hajawahi kutwaa taji lolote. Ana mbinu za kushinda mataji au kuiimarisha timu tu? hili ndio swali.
 
Akipewa nafasi kisha akapewa pesa, kuna uhakika wowote kwamba ana uwezo wa kuigeuza klabu yako kuwa ya mataji? Bado haina uhakika sana. hajawahi kufanya hivyo hapo kabla. Ndio maana bado inabakia kuwa bahati Nasibu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…