Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Edinson Cavani huenda akakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya vilabu bingwa dhidi ya Manchester United.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anauguza jeraha katika kiuno chake baada ya kufunga mkwaju wa penalti katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Bordeaux.
Mshambuliaji mwenza Neymar hatoshiriki katika mkondo wa kwanza wa mechi hiyo na ule wa pili mnamo tarehe 6 mwezi Machi.
 
Katika taarifa PSG imesema kuwa kutopatikana kwa Cavani kutategemea jeraha lake katika siku chache zijazo.
Akizungumza na runinga ya Ufaransa siku ya Jumapili, mkufunzi Thomas Tuchel alisema: Hakuna habari nzuri kuhusu Edi hii leo.
Aliongezea: Anafanyiwa vipimo hii leo katika kituo cha mazoezi, klabu itatoa taarifa baadaye , lakini kwa maoni yangu habari hizo haziridhishi. Itakuwa vigumu sana kumchezesha.
 
Kuna matumaini ya kiwango cha chini sana. Tuna matumaini lakini vipimo vya kwanza sio vizuri.
Mshambuliaji wa Brazil Neymar alipata jeraha katika ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa wa kombe la ligi nchini Ufaransa Strasbourg tarehe 23 Januari na hatoweza kucheza kwa wiki 10.
Hatua hiyo inamwacha mshindi wa kombe la dunia Kylian Mbappe-ambaye alichukua mahala pake Cavani wikendi iliopita.
 
Hatahivyo, Tuchel alisema kuwa kulikuwa na habari njema kwa mchezaji mwengine muhimu Marco Verratti, ambaye alishiriki katika mechi dhidi ya Bordeaux baada ya kukaa nje kwa wiki tatu na jeraha la kifundo cha mguu.
"Verratti anaweza kucheza na atacheza, alisema raia huyo wa Ujerumani . Nina wasiwasi kwasababu wachezaji muhimu wanauguza majeraha'' .
Kwa mechi kuu katika kombe la vilabu bingwa ni muhimu kuwa na wachezaji muhimu wenye uzoefu mwingi.
PSG iko pointi 13 juu ya ligi ya daraja la kwanza lakini ushindi wao dhidi ya Bordeaux ulijiri baada ya wiki ngumu .
 
Wanasayansi wamevumbua njia ya kumdhibiti mbu anayesababisha malaria kwa kutumia dawa iliyo na chembe chembe ya damu ya binadamu.
Dawa hiyo inaaminiwa kuwashibisha mbu na kuwafanya kukosa hamu ya kumuuma mtu, wamesema wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rockefeller nchini Marekani.
Mfumo huo wa tiba utakapo idhinishwa unaweza kutumika kuzuia homa ya zika, homa ya manjano na malaria.
 
Utafiti huo japo bado uko katika awamu ya kwanza uanatoa matumaini ya kupatikana kwa tiba ya magonjwa hayo hasa katika maeneo yanayowaathiri watu kwa wingi.
Mbu wa kike pekee ndio wanaouma watu na wanavutiwa sana na damu ya binadamu kwa sababu ina madini ya protini wanayohitaji ili kuzaana.
Watakapomuuma mtu aliyemeza dawa hiyo mpya inayofanyiwa uchunguzi watashindwa kufanya kazi kwa siku kadhaa.
 
Back
Top Bottom