Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23]
 
He!!!
 
Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Chile Alexis Sanchez, 30, anaweza kurudi Arsenal baada ya kushindwa kufanya vizuri Old Trafford, amesema mchezaji maarufu wa zamani wa klabu ya Arsenal Marc Overmars. (ADN Deportes - in Spanish)
 
Chelsea wanaamini kuwa wanaweza kumsajili moja kwa moja mshambuliaji raia wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, kwa chini ya euro milioni 36 kama walivyokubaliana na Juventus hapo awali. (ESPN)
 
Juventus wametoa ofa ya pauni milioni 44 na mshambuliaji wao Paulo Dybala, 25, kwa Liverpool ili wamsajili mshambuliaji hatari Mohammed Salah, 26. (Tuttosport, via Mail)
 
Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 45 kumsajili mshambuliaji wa Benfica na timu ya taifa ya Serbia Luka Jovic, 21, ambaye yupo kwa mkopo na klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani. (Bild - in German)
 
Beki wa kati wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, anataka kumfuata Mholanzi mwenzake kiungo Frenkie de Jong, 21, amesema mchezaji mwenzake Andre Onana. (Goal)
 
Hata hivyo, Barcelona hawawezi kutoka kitita cha pauni milioni 75 ili kumsajili beki huyo, hali inayoifanya Manchester City kuwa katika nafasi nzuri ya kumnyakua De Ligt. (Mail)
 
Manchester United wanataka wachezaji wao golikipa David de Gea, 28, na mshambuliaji Marcus Rashford, 21, kusaini mikataba mipya kabla ya msimu huu kwisha.(Goal)
 
Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois, 26, amesema kuwa anatamani kupata fursa ya kucheza tena katika ngazi ya klabu pamoja na mshambuliaji wa Eden Hazard ,28. Wawili hao wanachezea timu ya taifa ya Ubelgiji pamoja na walikuwa wote Chelsea, Hazard anahusishwa na uhamisho kuelekea Madrid kutokea Chelsea. (VTM Nieuws, via FourFourTwo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…