moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Ningendako.[emoji2][emoji2]View attachment 1023391
Simba ilikoswakoswa kushuka daraja, Kati mwaka 1987,1988 na 1989. Hii ilitokana na ugomvi binafsi wakati huo kati ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba kwa vipindi viwili tofauti na ambaye pia alikuwa Meneja utawala wa Shirika la Bima la Taifa, Jimmy David Ngonya na mfanyabiashara maarufu jijini Dar as salaam, ambaye naye aliwahi kuwa katbu mwenezi wa Simba kwa vipindi viwili tofauti, Hassan Juma Brashi.
Ugomvi wao inadaiwa ulitokana chuki za kiuongozi baina yao.
Hilo lilipelekea kuhujumiwa kwa Simba ili kumkomesha Ngonya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba wakati huo.
Naomba nikwambie, ukisikia Yanga imefungwa na Simba goli 4,5 au 6 jua ndani ya Yanga kuna mgogoro. Na upande wa Simba ni hivyo hivyo.
Mgogoro wa Simba kwenye miaka hiyo mitatu ilikua fursa muhimu kwa Yanga kulipa visasi vyote kwa Simba, lakini hilo halikutokea.
Ilikuwa kwamba Simba hata ikiwa na mgogoro wa uongozi ikifika mechi na Yanga, waliacha tofauti zao wanakuwa kitu kimoja. Yanga na Simba wakati huo walikua wanafungana kwa zamu ama sare.
Kwahiyo wakati huu tukikumbuka kipigo cha Simba 5-0 Yanga iwe chachu kwenu, jipangeni mlipe kisasi [emoji16][emoji16][emoji16]