Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JIFUNZE MBINU ZA MALEZI KUTOKANA NA MAKALA HII.


*Majirani wawili wote walikuwa wamepanda maua mazuri pembeni mwa nyumba zao, jirani mmoja alikuwa kijana mmoja Engineer na jirani mwingine alikuwa Mzee Mstaafu.*

Kijana Engineer yeye alikuwa anautunza maua yake vizuri sana kwa kuyamwaligilia maji vizuri, aliweka mbolea, aliweka madawa ya kuua wadudu, alipalilia vizuri maua yake na maua yake yalipendeza na kuleta mwonekano mzuri sana.

Mzee Mstaafu yeye alikuwa anamwagalia kwa nadra sana, hakuweza kuweka mbolea za kutosha pia, hakuwahi kabsa hata kupulizia madawa ya wadudu kwenye maua yake. Na maua yake yalionekana kuwa si mazuri ukilinganisha na ya jirani kwani maua ya jirani yalikuwa _Leafy, super green and luxuarant._ *Yaani siyo siri yalivutia kwa kila aliyeyatazama*

Siku mmoja mvua kubwa ilinyesha maua ya kijana engineer yote yalingolewa na mvua kubwa wakati Maua ya mzee mstaafu yakiwa salama hayajasombwa na mvua. *Kijana engineer alishangaa sana maua yangu yenye afya nzuri yamesombwa na mvua ya huyu Mzee yamebaki hiki ni kitu gani jamani mbona maajabu.*

_Kijana Engineer alimwuliza kwa nini Maua yangu yamebebwa na mvua wakati yangu yalikuwa mazuri kuliko yako, Mzee Mstaafu akajibu Maua yangu sikuyapa Maji ya kutosha kwahiyo kuna kipindi ilibidi mizizi yake iende chini zaidi ili kupata maji ya kutosha wakati maua yako yalipata kila kitu hivyo mizizi haikuwa imezama sana chini ndiyo maana imekuwa rahisi kubebwa na mvua._

*Unaweza ukawa hupati unachokihitaji leo kwenye maisha yako kumbe kitu hicho kinakuandaa kuwa mtu imara zaidi kesho ukikutana na changamoto utaweza kushinda bila hata kujua kumbe mapungufu ya jana ni nguvu ya kesho. Usilie na hali ya sasa bali inakuandaa kuwa mwenye kusimama kesho.*

*Malezi tunayowapa hata watoto wetu lazima yawe na uwiano bila hivyo tunaweza tukawa na watoto kama maua ya Kijana engineer changamoto ndogo tu chali kwa sababu ya hadhi na fahari zetu tunafikiri kuwajali sana na kuwadekeza ndyo malezi sahihi.*

[emoji1594][emoji1594]‍[emoji2382]Tusitarajie miujiza katika Ukomavu wa watoto wetu kupambana na changamoto za Kimaisha kama misingi ya Malezi tuwapatiayo ni legelege tangia utoto wao[emoji2992][emoji2992]


*Siku njema wana wa Mungu tuzidi kudumu katika sala. Kesho yetu ni njema sana kwa mapenzi ya Mungu*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…