Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alisema: “Inanichanganya kidogo kwa kile tunachotaka kiwe na kule tunakopanga kwenda. Ni kama mbio za farasi hujui mwisho wake ukoje, japo tuna matumaini ya kushinda.
 
Solskjaer yupo vizuri kwelikweli kwenye kikosi hicho cha Man United tangu alipoanza kukinoa, kwamba amepoteza mara moja tu na kushinda 11 katika mechi 13 alizowaongoza. Katika kuwakabili mahasimu wao hao wakubwa kabisa huko England, Ferguson amepewe nafasi ya kusema neno lake kwa wachezaji wa Man United.
 
Acha tuzibangue wenyewe,tutaziuza rejareja mtaani.
a6a02a6f1cc50d8f3ef7ab9308340a0d.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majibu yaliyopatikana ni kwamba ngoma droo. Man United makali yao yapo golini na kwenda kiungo, wakati Liverpool wao ni kwenye beki na fowadi. Ukihesabu wachezaji, Man United imeingiza watano, wakati Liverpool wao wameingiza wachezaji sita kwenye kikosi hicho cha pamoja.
 
Vigogo hao wawili wanapokutana, unaambiwa ni mshikemshike. Lakini, kama ingeamriwa kupangwa kikosi kikosi kimoja, piga au, David De Gea wa Man United lazima aanze na kumweka beki Alisson Becker wa Liverpool. Shughuli wa De Gea hakuna asiyeifahamu ni hutarajii kuona akishindwa kupata namba katika kikosi chochote kile duniani kwa sasa.
 
Kwenye safu ya ulinzi, Man United inaingiza mtu mmoja tu, beki wa kati Victor Lindelof, ambaye atacheza sambamba na Virgil van Dijk kwenye sehemu hiyo, wakati mabeki wa pembeni kulia na kushoto wote ni wa kutoka Liverpool, Trent Alexander-Arnold na Andrew Robertson mtawalia. Kwenye safu ya ulinzi ya kikosi hicho, Luke Shaw na Erick Baily itabidi wasubiri tu kwenye benchi.
 
Katika safu ya kiungo, kikosi hicho ambacho kitatumia fomesheni ya 4-3-3, Man United imeingiza viungo wawili, Ander Herrera na Paul Pogba, ambao watacheza sambamba na staa wa wa Liverpool, Georginio Wijnaldum. Kwenye eneo hilo, Nemanja Matic na Naby Keita itabidi tu wasubiri kwenye benchi sawa na ilivyo kwa Jordan Henderson na viungo wengine kutoka kwenye vikosi vya wababe hao.
 
Kwa idadi ya wachezaji 11 wanaopaswa kuanza, Man United imeingiza wachezaji watano kwenye kikosi hicho, wakati Liverpool yenye ikiingiza sita, huku Jurgen Klopp kikosi chake kikiwa na nguvu zaidi kwenye mabeki na washambuliaji, wakati Solskjaer timu yao ikiwa na nguvu kwenye sehemu ya kiungo na golini kwa kipa De Gea.
 
Hapana. Sidhani kama Jurgen Klopp atasoma ninachokisema. Kwa sababu sitasoma atakachosema au wachezaji wake watakachokisema. Namkaribisha tu Ferguson kuja kusema maneno yake kwa sababu nafahamu ni furaha kiasi gani anakuwa nayo pindi Man United inapoichapa Liverpool. Wachezaji wetu wanafahamu pia kuwafunga Liverpool kuna maana kubwa sana kwa kila mtu wa Man United,” alisema Solskjaer.
 
Back
Top Bottom