Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lionel Messi (Barcelona)

Asikwambie mtu, mashabiki wa soka hawajawahi kutosheka katika maisha yao. Cheki hata Lionel Messi kuna nyakati anakumbana na wakati mgumu wa kuzomewa na mashabiki wa Barcelona.

Katika mechi ambayo Barcelona alichapwa 4-0 na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Messi alikumbana na wakati mgumu kuzomewa na mashabiki wake mwenyewe. Staa huyo matata kabisa kwenye kikosi cha Barcelona, alikuwa na wakati mgumu kwenye mechi dhidi ya Leganes iliyofuatia baada ya kipigo hicho cha kutoka kwa PSG.
 
Kwenye mechi hiyo ya Leganes, uwanjani Nou Camp, Messi alizomewa kila alipogusa mpira, lakini hakujali alifunga bao la ushindi dakika za mwisho, Barcelona wakishinda 2-1. Hata hivyo alizomewa hadi mechi ilipomalizika alipokuwa akienda vyumbani.
 
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Supastaa, Cristiano Ronaldo aliwahi kusema kwamba anawaheshimu sana mashabiki wa Manchester United kwa sababu hawajawahi kumzoea kwa kipindi chake alichokuwa kwenye timu hiyo.
 
Hali haikuwa hivyo alipokuwa huko Real Madrid, licha ya kwamba aliwatendea mengi mazuri ndani ya uwanja, lakini mashabiki wa timu hiyo bado walimzomea. Katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich na Los Blancos ilishinda mabao ya jumla 6-3, huku Ronaldo akifunga mabao matano kati ya hapo, lakini mashabiki wa timu yake hawakusita kumzomea na kupiga miluzi katika mechi iliyofanyika Santiago Bernabeu kila alipogusa mpira.
 
Wayne Rooney (Man United)

Mwaka 2010, Wayne Rooney aliomba kuihama Manchester United na hakika jambo hilo liliwakera sana mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. Rooney aliomba radhi na kisha kupewa mkataba mnono, lakini mashabiki hawakumwacha salama.
 
Kilichowakera mashabiki wa Man United kwa wakati huo kwamba Rooney alikuwa akitaka kuondoka kwenye timu yao akajiunge na Manchester City. Mechi zilizofuatia baada ya hapo, Rooney alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuzomewa na mashabiki kwenye mechi za Old Trafford hadi hapo alipoomba radhi na kusamehewa kisha ya kuwafanya mashabiki hao hata kusimama kumpigia makofi wakati aliporudi uwanjani hapo akiwa na kikosi chake cha Everton.
 
Mauro Icardi (Inter Milan)

Straika, Mauro Icardi kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu katika kikosi cha Inter Milan huko Italia kufuatia kuvuliwa unahodha na kuwekwa benchi baada ya kuwapo na shida kwenye mambo ya mkataba mpya. Lakini, huko nyuma straika huyo ambaye amekuwa akiwafungia Inter mabao mengi tu kwa kila msimu, aliwahi kuwa kwenye kipindi kigumu sana cha kuzomewa na mashabiki wa timu yake mwenyewe.
 
Hilo lilitokana na kitendo chake cha kukosa penalti katika mechi dhidi ya Cagliari na baada ya hapo likamfanya awe adui wa mashabiki hao. Kwenye kitabu chake alichotoa mwaka 2016, Icardi aliwashambulia mashabiki hao waliokuwa wakimzoea kitendo kilichomfanya uongozi wake wa klabu ya Inter kumtoza faini. Icardi alidai mashabiki hao wasivyompenda walidiriki hadi kushangilia alipokosa penalti.
 
Gareth Bale (Real Madrid)

Supastaa, Gareth Bale haonekani kama atakuja siku akawa kipenzi cha mashabiki wa Real Madrid kwa sababu hajawahi kuwa mtu wao. Winga huyo wa kimataifa wa Wales mara kadhaa amejikuta kwenye wakati mgumu na kuzomewa na mashabiki wa timu yake.
 
Bale licha ya kwamba alifunga mabao muhimu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini jambo hilo halijawahi kufaa na kumwokoa kwenye zomeazomea ya mashabiki wa timu hiyo.

Sasa tangu Cristiano Ronaldo alipoondoka kwenye timu hiyo kwenye Juventus mwaka jana, chuki za mashabiki wa Los Blancos dhidi ya Bale zimeongezeka maradufu zaidi kiasi cha kumfanya staa huyo ashauriwe kuhama kwenye timu hiyo na kwenda kujiunga na timu nyingine.
 
Marouane Fellaini (Man United)

Kiungo, Marouane Fellaini mara kadhaa alijikuta kwenye wakati mgumu mbele ya mashabiki wake mwenyewe wakati alipokuwa katika kikosi cha Manchester United. Kuna mechi moja ambayo Fellaini alianzia benchi na kuingia dhidi ya Spurs, mashabiki wa Man United walionekana kutopendezwa na jambo hilo na kuanza kumzoea staa huyo wa Ubelgiji.
 
Fellaini ulikuwa usajili wa David Moyes kwenye kikosi hicho cha Old Trafford na tangu mwanzo tu hakuwa kwenye mioyo ya mashabiki wa Man United, kwani mwaka 2016, walimzoea hata kabla ya mechi, huko Old Trafford wakati wachezaji walipokuwa wakipasha misuli moto.
 
Kwenye mechi ya Spurs aliyoingia akitokea benchi alizomewa, kwa sababu wiki moja iliyopita, akiingia kutokea benchi alisababisha penalti na kuwafanya Everton kupata sare ya 1-1. Kwa sasa Fellaini ameuzwa kwenda China na hilo limewafurahisha sana mashabiki wa Man United.
 
Romelu Lukaku (Ubelgiji)

Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku aliwahi kukumbana na balaa la kuzomewa wakati alipokuwa akiichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji. Mashabiki waliokuwa wakimzomea ni wa Ubelgiji. Lukaku alikuwa kwenye shida hiyo kisa tu alikosa bao la wazi kwenye mechi dhidi ya Bosnia. Straika
 
Lukaku ilibidi asubiri hadi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 na alifunga mabao manne katika fainali hizo na kuwasahaulisha mashabiki zile kelele juu yake kwenye suala la kukosa nafasi nyingi za kufunga na kutupia wavuni mara chache. Lukaku alisaidia timu yake ya Ubelgiji kushika nafasi ya tatu katika fainali hizo zilizofanyika Russia.
 
Not looking good eeeeh!?
Screenshot_20190224-100903~2.jpeg
 
Back
Top Bottom