Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipa Kepa Arrizabalaga ametozwa faini ya thamani ya mshahara wa wiki moja na ameomba msamaha kwa kukataa kuondolewa uwanjani wakati a mechi ya fainali ya taji la Carabao wakati timu hiyo ilipofungwa na Manchester City Jumapili.
Mchezaji huyo raia wa Uhispani alikataa akuondolewa uwanjanai na kipa wa ziada Willy Caballero kuichukua nafasi yake katika uwanja wa Wembley.
 
Licha ya kwamba hatukuelewana, kwa kujitathmini, nilifanya makosa kwa namna nilivyoshughulikia hali hiyo ," Kepa amesema katika taarifa rasmi ya Chelsea.
Meneja Maurizio Sarri amesema kwamba yeye na Kepa wamekuwa "na mazungumzo mazuri".
 
Sarri, aliyeondoka kwa hasira wakati Kepa alipokataa kutoka uwanjani kuikia dakika za mwisho za muda wa ziada , pia amebaini kwamba 'hawakuelewana'.
Lakini aliongeza: "Kepa ametambua alifanya makosa makubwa katika namna alivyofanya.
"Ameniomba msamaha, amewaomba wachezaji wenzake na timu nzima kwa jumla msamaha. Ni uamuzi wa klabu hiyo iwapo watataka kumuadhibu kwa mujibu wa sheria za klabu, lakini binafsi, suala hili limemalizika.
 
Uchezaji wa timu nzima kwa jumla, ulikuwa ni matumaini makubwa na ni aibu kuona namna tukio hili limegubika mchezo wa na jitihada za timu katika fainali iliyokuwana ushindani mkubwa."
Kepa, ambaye ni mchezaji wa klabu hiyo aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa £71m, alikaidi jitihada za Sarri kumuondosha uwanjani na kumuweka kipa mwenza Caballero kabla ya Manchester City kushinda kwa penalti. Raia huyo wa Italia alionekana na haisra kubwa na aliondoka uwanjani kabla ya muda mfupi kurudi tena
 
Hivi sasa Ulaya yote ni Mohamed Salah, Sadio Mane wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang na Alex Iwobi wa Arsenal ambao wanatamba hawa walifanya makubwa kwa kipindi kirefu na kugeuka mifano kwa vijana wanaochipukia kwenye soka.
 
Hivi sasa Ulaya yote ni Mohamed Salah, Sadio Mane wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang na Alex Iwobi wa Arsenal ambao wanatamba hawa walifanya makubwa kwa kipindi kirefu na kugeuka mifano kwa vijana wanaochipukia kwenye soka.
 
Jay Jay Okocha

Okocha alikuwa maarufu kwa ‘vyenga’. Alikupiga chenga na kisha anakucheza, ilikuwa staili yake wakati mwingine. Aliwahi kutwaa Tuzo ya mchezaji Bora Nigeria mwaka 1995, 1997, 2000, 2002, 2003, 2004 na 2005. Jina lake hasa ni Augustine Azuka Okocha lakini wengi wanamtambua kama Jay Jay Okocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…