Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kamera zilionyesha tukio kwa ufasaha huku Arrizabalaga akigoma kutoka nje na Sarri aliyekuwa kando ya msaidizi wake, Gianfranco Zola wakimsisitizia kutoka. Baadaye mwamuzi wa akiba alishusha bango la kubadilishia wachezaji huku Sarri akipandwa na hasira na kutokomea katika vyumba vya kubadilishia nguo huku mechi ikiendelea.
 
Kitendo cha Kepa kumgomea Sarri kimeshambuliwa na wachambuzi mbalimbali wa soka na mashabiki hasa mitandaoni, lakini Sarri amejaribu kushusha pumzi akidai kwamba kulikosekana maelewano yaliyopeleka Arrizabalaga agome kutoka nje.
 
Nilielewa kulikuwa na tatizo na tulihitaji mabadiliko. Lakini nikafahamu kilichotokea wakati daktari alipokuja baada ya dakika nne. Kulitokea kutoelewana. Nilijua kipa alikuwa ameumia kwahiyo asingeweza kwenda katika kudaka penalti. Hata hivyo kumbe hakuwa na tatizo na angeweza kudaka penalti.” Alijitetea Sarri.
 
Kuhusu maamuzi yake ya kwenda katika chumba cha kubadilishi nguo huku mechi ikiendelea, Sarri alisema β€œNilihitaji utulivu kidogo. Kama nilivyosema nilidhani kipa alielewa nilitaka mabadiliko kwa sababu ya hali yake ya kimwili, na alisema hana matatizo ya mwili. Kwahiyo nadhani nilikuwa sahihi.”
 
Naye Arrizabalaga ambaye alinunuliwa kwa rekodi ya uhamisho ya dunia ya makipa dau la Pauni 75 milioni kutoka Athletic Bilbao dirisha kubwa lililopita la majira ya joto alidai hakuwa na lengo la kumdharau kocha wake.
 
Sijui ilikuaje lakini haijaleta picha nzuri. Nimeongea na bosi. Nadhani ilitokea kutoelewana. Naelewa televisheni na mitandao ya kijamii wanaongelea jambo hili lakini nipo hapa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kusema halikuwa dhumuni lake kumpinga kocha. Tumeongea sasa hivi na najaribu kusema tuko poa. Alidhani halikuwa jambo zuri. Kilikuwa kipindi kigumu na mambo mengi utokea,” alifafanua kipa huyo.
 
Staa wa zamani wa Newcastle na timu ya taifa ya England, Alan Shearer ambaye alikuwa akichambua mechi hiyo alipinga madai ya Sarri kwamba kulitokea na kutoelewana kati yake na Arrizabalaga na badala yake akadai kocha huyo anajua kuwa alidharauliwa na mchezaji wake.
 
Nadhani habari inajieleza yenyewe jinsi ambavyo kocha alikasirika. Alikuwa kama mwendawazimu. Sidhani kama ni suala la kutoelewana. Alitaka kumtoa kipa kwa sababu fulani lakini kipa akaamua kutomtii na kumdharau,” alisema Shearer.
 
Naye staa wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uholanzi, Ruud Gullit ambaye alikuwa akichambua pambano hilo sambamba na Shearer alidai Sarri alikuwa ametoa ufafanuzi wa β€˜kisiasa’ kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo katika vyombo vya habari.
 
Staa mwingine wa zamani wa England, Chris Sutton ambaye alicheza sambamba na Shearer katika kikosi cha Blackburn Rovers kilichotwaa ubingwa wa England mwaka 1995 alidai Arrizabalaga hastaili kuichezea tena Chelsea kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…