Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakuu kuna hii habari..
tapatalk_1551201559274.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANZIA : Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ltd. Ruge Mutahaba amefariki Dunia jioni ya leo nchini Afrika Kusini. Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema peponi..
 
GHAFLA, jina la Arsene Wenger limeibuka na kuhusishwa na mpango wa kwenda kuwa kocha wa Leicester City baada ya Claude Puel kufutwa kazi wikiendi iliyopita. Sambamba na Wenger, ambaye kwa sasa yupo tu akiwa hana kazi ya ukocha tangu alipoachana na Arsenal, kocha mwingine anayetajwa na kupewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya King Power ni Brendan Rodgers.
 
Rodgers, anayeinoa Celtic aliwahi kutamba Ligi Kuu England akiwa na vikosi vya Swansea City na Liverpool, hivyo Leicester wanadhani anaweza kutosha kwenye kuinoa timu yao.
 
Leicester City haijapata ushindi wowote katika mechi saba za mwisho na wanashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi, huku kocha Puel alikuwa ameshinda mechi nne tu kati ya 13 alizocheza King Power, huku akichapwa kwenye mechi saba, zikiwamo nne za mwisho alizokumbana na vipigo mfululizo.
 
Wachezaji Kamari wameanza kuhusisha majina ya makocha ambao wanaamini wanaweza kutua huko King Power, huku Rodgers akiongoza na kufuatiwa na makocha wengine kadhaa akiwamo David Wagner, Rafa Benitez, Sean Dyche, Sam Allardyce na Wenger.
 
Makocha wengine ambao wanatajwa kwenda hapo ni Harry Redknapp, Nigel Pearson, Leonardo Jardim, Mikel Arteta, Neil Lennon, Marcelo Bielsa, Gary Rowett, Thierry Henry, Carlos Carvalhal, Mark Warburton, Michael O’Neill, David Moyes, Alan Pardew, Chris Coleman na Roberto Martinez.
 
Back
Top Bottom