Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dharau za kocha huyo wa muda wa Manchester United zinakuja baada ya kukabiliana na Liverpool na kutoka nayo sare ya bila kufungana, huku kwenye mechi hiyo kikosi chake kikiwa kimewakosa mastaa kibao muhimu kutokana na kuwa majeruhi.
 
Kwenye mabadiliko yake, Solskjaer aliwaingiza wachezaji Andreas Pereira na Alexis Sanchez. Pereira alikuja kucheza kwenye kiungo na kinda mwenzake, Scott McTominay, ambaye alianza kwenye mechi hiyo kutokana na Nemanja Matic kuwa majeruhi.
 
Baada ya mechi, mashabiki wa Man United waliwakejeli Liverpool, wakiwaambia kama wameshindwa kupata ushindi kwenye timu hiyo, basi hawawezi kupata tena kwani kikosi kizima cha kwanza kilikuwa nje, huku wakitamba kwa kiwango kile, timu yao ina vikosi viwili moto, wanaoanza na wale wanaokaa benchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…