Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya mechi, mashabiki wa Man United waliwakejeli Liverpool, wakiwaambia kama wameshindwa kupata ushindi kwenye timu hiyo, basi hawawezi kupata tena kwani kikosi kizima cha kwanza kilikuwa nje, huku wakitamba kwa kiwango kile, timu yao ina vikosi viwili moto, wanaoanza na wale wanaokaa benchi.
 
Man United ina majeruhi 10 kwenye kikosi chake, wachezaji tisa panga pangua hawakosekani kwenye kikosi cha kwanza, ambao ni Matteo Darmian, Ander Herrera, Phil Jones, Lingard, Anthony Martial, Mata, Matic, Marcus Rashford, Antonio Valencia na Mason Greenwood.
 
Hiyo ni timu nzima ipo nje ya uwanja. Lakini Solskjaer anaamini kwenye kikosi chake kuna mastaa wengine matata kabisa ambao wamekuwa wakikaa benchi, watatumika kuleta matokeo bora uwanjani. Ukiwajumuisha McTominay na Perreira, Ole anawagemea pia wakali wengine kama Fred, Tahith Chong, Jimmy Garner na Angel Gomes, ambao wataingia kwenye kikosi kuungana na wakali wa siku zote, David De Gea, Ashley Young, Chris Smalling, Victor Lindelof, Luke wLukaku, Eric Bailly, Sanchez, Diogo Dalot na Sergio Romero kusukuma jahazi.
 
Jana wamecheza vzr sana,sikutegemea kupata matokeo kama yale,,Ole anapaswa kupongezwa aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…