Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1551367173668.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UONGOZI NA KIONGOZI

Uongozi unajumuisha yafuatayo: Nini cha kufanya, wapi na lini na Kwa njia IPI , Mpango Kazi na mpango mkakati, sifa za mtendaji na jinsi ya kutathimini malengo yaliyokusudiwa nk

Kiongozi ni mtu yeyote mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi juu ya jambo lolote na kulisimamia ili kufikia lengo lilokusudiwa Kwa manufaa ya kikundi/familia/taasisi nk

Kiongozi huandaliwa ili kuweza kuyatekeleza masuala yote ya uongozi kwa kupewa elimu (semina/ kozi mbalimbali) pamoja na uzoefu wa kimaisha na elimu ya mitaani.

Watu husema uongozi ni kipaji anachozaliwa nacho MTU. Ni kweli, lakini si kwa wote. Wale wenye vipaji huhitaji kuendelezwa ili viweze kutumika vizuri ktk utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo yaliyopangwa.

Kiongozi bora ni yule anayetekeleza majukumu yake Kwa kufuata kanuni,taratibu na sheria (maadili ya Kazi) ipasavyo. Huwa hatetereki katika kusimamia haki bila kutetereka.

Uongozi bora ni pale ambapo masuala yote ya uongozi yametekelezwa kwa ukamilifu bila ukiukwaji wa aina yoyote. Hivyo uongozi mbaya unategemea mambo makuu mawili

Kwanza, masuala ya uongozi kama ni hasi, na kwa vile kiongozi anapaswa kutekeleza kama yalivyo, basi, matokeo huwa ni hasi (hapa kiongozi halaumiwi)

Pili, pale ambapo kiongozi anashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa sababu yo yote ambayo iko chini ya mamlaka yake, matokeo huwa ni hasi (hapa kiongozi hulaumiwa)

Hivyo basi kiongozi na uongozi ni vitu viwili tofauti vinavyotengemeana kufikia uongozi bora. U kiongozi bora katika familia yako? Kazini kwako? Group lako la Whatsapp? Uzi wa likes? TRM?

[emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488]
 
Lady Jay Dee aliandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Ilikuwa siku ya Jumatano, tarehe moja mwaka 2013.

WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki. Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mawe. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu. Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.

Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..

Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.

Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili. Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu. Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo?? Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.

JIDE
 
Na mimi ndio nilikua nasikia hivyo pia ndio ukweli ulivyokua lakini kwa nilivyomuona leo naona hali ni tofauti, jamaa yupo rafu sana, yupo tungi alafu anatoa zile tano zake kwa kila mtu mixer kupiga mistari hadharani. nahisi life limekua gumu upande wake
Aisee,inasikitisha sana,,nafikiri ni life labda lmemchanganya pelekea na kile kifo cha mchumba wake,,hali ni mbaya sana,,ni kumuomba Mungu tu
 
Back
Top Bottom