Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara ya kwanza kuwafunga ilikuwa kwenye fainali ya michuano hiyo msimu wa 2013/14. Misimu miwili iliyofuatia, hakuwafunga, kabla ya kuja kuwapiga hat-trick kwenye nusu fainali msimu wa 2016/17 na kika kuja kuwafunga tatu nyingi Jumanne iliyopita, safari hii akiwa na Juventus.
 
2. Bayern Munich – mabao 9

Bayern Munich na Real Madrid ni timu mbili zenye rekodi nzuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na jambo hilo zimelifanya timu hizo kuwa mahasimu wakubwa wanapokutana uwanjani. Lakini, wababe hao wa Ujerumani ni miongoni mwa wahanga waliofungwa mara nyingi na supastaa Ronado katika mechi za michuano hiyo ya Ulaya.
 
Katika nusu fainali ya 2011/12, Ronaldo alifunga mara mbili kwenye mechi ya marudiano, lakini alishindwa kuifikisha timu yake fainali. Msimu wa 2013/14, alirudia yake makali yake akifunga mara mbili pia kwenye nusu fainali ya pili. Misimu mitatu baadaye walikutana kwenye hatua ya robo fainali na Ronaldo alifunga mabao matano katika mechi mbili walizocheza hatua hiyo.
 
1. Juventus – mabao 10

Kuna ile wanayosema, kama huwezi kumpiga basi uungana naye. Hilo ndilo walilofanya Juventus kwa Cristiano Ronaldo kwa kuamua kumsajili maana amewapiga sana kwenye mechi alizowahi kukutana nao. Katika nyakati zake alizokuwa kwenye kikosi cha Real Madrid, timu hiyo ilikutana na Juventus mara kadhaa na mara zote Ronaldo alikuwa akiweka mpira kwenye nyavu.
 
Ronaldo amecheza mechi saba dhidi ya Juve na amefunga kwenye mechi zote hizo, akiweka kwenye kamba mabao 10, mabao matatu yalikuwa kwenye hatua ya makundi msimu wa 2013/14, mawili kwenye nusu fainali 2014/15, mawili kwenye fainali 2016/17 na matatu mengine kwenye robo fainali 2017/18.
 
Msimu huu Man City wapo kwenye mchakamchaka wa kubeba mataji mane, wakiwa tayari wameshanyakua Kombe la Ligi, jana Jumamosi wamefuzu kwa nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kuichapa Swansea mabao 3-2 katika mchezo wa robo fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…