Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilikuwa naona unapita kimya, nilishangaa ila sikuogopa maana uliwahi fanya hivyo huko nyuma, karibu tena tuburudike
Kugonga likes ni rahisi kuliko kuanza kufukunyua vitu kuposti. Unagonga likes wakati wa break halafu huyoo unatia simu mfukoni unarudi kwenye majukumu.

Nimepitwa na nini? Hakuna aliyetushambulia ile kanda pendwa nihangaike naye? [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hapa uliongoni tuko vizuri, sidhani kama kuna kipya labda kwakuwa wakati furani nakuona unapendelea udaku huenda wadau wa udaku watajibu.
Habari kubwa jamiiforums ni mwanasiasa mkongwe, Waziri Kiongozi mstaafu, muasisi wa mageuzi , mmoja wa waasisi wa ukawa, Seif Sharrif Hamad , ajiondoa CUF na kujiunga na ACT Wazalendo na kuviacha vyama 3 vya CHADEMA, NCCR Mageuzi na NLD ambavyo alishirikiana navyo kuunda Ukawa.
 

Eti "...kwa kuwa wakati furani nakuona unapendelea udaku...". Umenichekesha sana aisee. Udaku una raha zake hasa ukiwa na siteresi. Angalizo tu ni kutokuufakamia sana vinginevyo utajikuta umepachikwa umama au uanaume wa Dar [emoji16][emoji16][emoji16]

Hayo ya wanasiasa wala hayashangazi. Wapo kazini kutafuta ugali na hakuna jipya. Kesho na keshokutwa utawasikia tena wamegeuza gia angani na kutenda kinyume na sasa. Hawafai !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…