Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ha hah

Hizo story zisikucheleweshe!! Ulikuwa muda wa kahawa ule.
Kuna watu humu wanatunza kumbukumbu balaa. Mimi hii misambwanda hii inanikosti mno. Hata nikimsalimia tu demu hapa JF basi utasikia "we mpenda misambwanda wewe utakuwa hujatulia wewe". Ifike mahala watu watofautishe porojo za kwenye kahawa na maisha halisi bana...Go bro [emoji109][emoji109][emoji109]
 
10. Welbeck (Arsenal)

Ni wazi kuwa, kama Arsenal ingeendelea kuwa chini ya utawala wa Arsene Wenger, Danny Welbeck butu kama alivyo, asingekuwa katika hali aliyonayohivi sasa. Mkataba wa Welbeck ungekuwa salama.

Wenger aliwajali wachezaji wake, hasa wale walio majeruhi kama Welbeck. Bila kupepesa, kuna sababu ya kurefusha mkataba wa straika huyo wa zamani wa Man United. Uwepo wake tu, unaongeza wigo wa wachezaji.

Mabao yake 32 katika michezo 126, akiwa na jezi ya Arsenal, ni ushahidi kuwa ni mfungaji mzuri kama sio hatari. Ni risasi ya akiba katika bunduki za washika mitutu hao wa London Kaskazini.
 
9. Olivier Giroud (Chelsea)

“Haiwezekani” hilo lilikuwa jibu la Mfaransa huyo alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuongeza mkataba katika klabu yake ya sasa ya Chelsea.

Olivier Giroud, amesoma alama za nyakati. Ni wazi kuwa, kwa sasa Maurizio Sarri, hana mpango naye kivile.

Licha ya kufunga mabao tisa, kwenye mechi tisa za Ligi ya Europa, Giroud hajaanza katika mchezo hata mmoja wa EPL, mwaka huu. Katika

umri wake wa miaka 32, straika huyo, anahitaji nafasi ya kudumu kwenye

kikosi cha kwanza.

Amekuwa akihusishwa na mipango ya kurudi kwao Ufaransa, lakini huenda Wachina

wakaleta ofa kubwa kuliko klabu ya Marseille inayoongoza mbio za

kuhitaji saini yake, ofa ambayo bila shaka yoyote ile, lazima

ataichukua na kuhitimisha miaka saba ya kucheza soka nchini England.
 
8. Mario Balotelli (Marseille)

Ndio kwanza ana miaka 28. Mkataba wake wa mwaka mmoja na klabu ya Marseille, aliyojiunga nao mwezi Januari mwaka huu, unamalizika mwisho wa msimu. Lakini mpaka sasa, Super Mario, hajapata Ofa ya kuongezewamkataba.

Amefunga mabo matano, katika mechi nane na kuthibitisha bado yuko fiti. Kiwango anachoonesha ni ishara kuwa, ni swala la muda tu na Muitaliano huyo, atarejea katika makali yake ya zamani, lakini swali ni Je, klabu gani iko tayari kumvumilia?
 
7. Hector Herrera (Porto)

Tottenham na Arsenal, walikuwa wanahusishwa na mpango wa kuitaka saini ya nahodha huyu wa FC Porto, lakini ripoti kutoka nchini Hispania, zinaonesha kuwa, kiungo huyo wa Mexico, ameamua kuelekea Atletico Madrid.

Uamuzi wa Hector Herrera, unaweza ukawa na maana kwani, kuna tetesi zinazomhusisha Saul Niguez na mpango wa kujiunga na Manchester City, katika dirisha la usajili la majira ya joto.
 
6. Juan Mata

(Man United)

Zaidi ya mara moja, Mhispania huyu, amekunukuliwa akisisitiza kuwa, hana shaka na mkataba wake unaomalizika mwisho wa msimu huu. Kiungo huyo mchezeshaji wa Man United, hayupo katika mipango ya Ole Gunnar Solskjaer.
 
5. David Luiz

(Chelsea)

“Nipo katika mazungumzo na uongozi wa klabu, kila mtu anafahamu ni jinsi gani ninavyoipenda Chelsea. Nikiwa hapa najihisi niko nyumbani,

nina furaha sana.” Hii ni kauli ya beki wa kati wa Chelsea, David Luiz, alipouliza kuhusu mustakabali wake.

Mkataba wa Luiz, mwenye miaka 31, aliyerejea Stamford Bridge, akitokea

PSG, unamalizika mwisho wa msimu, lakini mpaka sasa ni ngumu kung’amua kama The Blues watakuwa tayari kumpatia mkataba wa mwaka na nusu
 
4. Diego Godin

(Atletico Madrid)

Baada ya miaka tisa, taji moja la La Liga, mataji mawili ya Kombe la Europa, medali mbili ya mshindi wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mkurugenzi wa ulinzi wa kikosi cha Atletico Madrid ya Diego Simeone, anatarajia kuondoka mwishoni mwa msimu.

Kuna tetesi kuwa, kuna mazungumzo ya chini ya kapeti, kati ya wakala wake na Manchester United. Hata hivyo, pia inadaiwa kuwa, kutokana umri wake mkubwa wa miaka 33, beki huyu kisiki wa Uruguay, anafikiria kutua Inter Milan.
 
3. Yacine Brahimi (Porto)

FC Porto, wapo katika wakati mgumu. Ndio na hilo halina ubishi. Hii ni moja ya klabu bora barani Ulaya. Wameingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Tatizo ni wachezaji. Wachezaji wanapenda kwenda kwenye vilabu vya ligi tano bora za Ulaya na sio huku.
 
Baada ya miaka mitano, winger wa Algeria, Yacine Brahimi, yuko mbioni kuondoka. West Ham, Newcastle na Everton, zote zinamhitaji, lakini kuna uwezekano mkubwa Brahimi kuelekea Serie A, ambako Lazio na Inter Milan wanatajwa kumtolea macho.
 
Mwenyewe nime pause kwanza kutafakari hili, sikujua kama angekua na hilo kichwani sababu ilikuwa discusssion ya watu watatu tu. Nmeshangaa sana!! Kuna watu wanatusoma na wanatuchukua kama walivyo tusoma, hii ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…