*_Baba kutoka mashambani alipata safari ya kwenda Mombasa kwa biashara. Baada ya wiki moja akampigia simu mtoto wake kujulia hali ya nyumbani._*
Baba: Alooo! Vipi hali zenu huko?
Mtoto: *Tuko poa Baba, kila kitu sawa isipokua kidogo tu kulitokea shida*
Baba: Shida gani??
Mtoto: *Waujua ule ufagio wenye gongo refu? Basi lile gongo lake lilivundika.*
Baba: Aaaah umenishtua, sineno tutanunua mwengine. Lakini nnani alouvunja?
Mtoto: *Ni ngombe wetu aliuangukia*.
Baba: Ngombe??
Mtoto: *Naam alikua anakimbia kwa khofu maana zizi lilikua limeshika moto..*
Baba: Ah moto! Lakini ngombe yuko salama?
Mtoto: *Hapana baba ng'ombe alikufa*.
Baba: Lahaulaaaa..... na ilikuaje zizi likashika moto?!
Mtoto: *Kwa hakika moto ulianza kwa nyumba yetu ukaenea mpaka ukafika zizini.*
Baba: Nyumba yetu imeshika moto??
Mtoto: *Ndio Baba wajua yote ni huyu ndugu yangu Juma mungu amrehemu*.
Baba: Mungu amrehemu?! Kwani mwanangu Juma amekufa?
Mtoto: *Ndio Baba Juma amekufa. Wajua alikua avuta sigara chumbani kwake sigara ikaanguka kwenye godoro na yeye amelala. Moto nyumba nzima.*
Baba: Wanambia Juma siku hizi avuta sigara! Alianza lini mambo hayo?
Mtoto: *Alianza wiki hii tu kwa sababu ya stress na huzuni nyingi tangu mama afe.*
Baba: Mtumeeeee, mamako pia amekufa??
Mtoto: *Ndio Baba lakini usijitie stress sana baba kama ni ufagio wallahi tutapata tu mwengine.*
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
°•°Faith •Hope •Charity•°•