Hangover ni nini?
Daktari kutoka Kituo cha Elimu na Tiba, Mloganzila (Muhas), Shindo Kilawa anasema, “hangover ni mkusanyiko wa dalili zinazotokana na kunywa pombe kwa kiasi kilichopitiliza, dalili hizo ni kama vile kichwa kuuma, kichefuchefu, kutapika, mwili kukosa nguvu, kutetemeka, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi na nyinginezo.”