Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ULE mchakamchaka wa Ligi Kuu England utaendelea tena usiku wa leo Jumanne na kesho Jumatano, wakati Manchester United na Manchester City zitakapohitaji kufanya mabadiliko mengine kwenye msimamo wa ligi hiyo.
 
Usiku wa leo, Man United itakuwa ugenini kwa Wolves ikijaribu kusaka matokeo ya ushindi ili kuendelea kung’ang’ania ndani ya Top Four, huku Man City nayo ikisubiri hadi kesho wakati itakapokuwa nyumbani kuikaribisha Cardiff City katika harakati zake za kurudi kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo na kuiengua Liverpool.
 
Mikikimikiki hiyo ya Ligi Kuu England imefikia patamu kwa sasa, pale kwenye Top Four na kwenda mbio za ubingwa hakuna anayehitaji kupoteza mchezo wake jambo linalofanya msimamo wa ligi hiyo kubadilika kila kunapokuwa na mechi zinazohusu vigogo waliopo kwenye Top Six.
 
Chelsea nayo itavuruga zaidi msimamo wa ligi hiyo kama hiyo kesho itashinda mechi yake dhidi ya Brighton itakayopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
 
Tottenham Hotspur ambayo kasi yake kwa sasa imekuwa ya kuchechemea nayo itakuwa kibarua kuikabili Crystal Palace kwenye uwanja wake mpya na kama itaendelea kufanya hovyo, basi bila ya shaka hadi kufikia Alhamisi asubuhi itakuwa imeshushwa hadi kwenye nafasi ya sita huko kama Man United, Chelsea na Arsenal zitakuwa zimeshinda mechi zao.
 
Mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaofanyika leo Jumanne, Watford itakuwa na nafasi ya kupoza machungu ya kuchapwa kwenye mchezo wa kwanza kwa kushuka uwanjani kwao kuikaribisha Fulham, ambayo ipo kwenye mapambano makubwa ya kujinusuru kwenye hatari ya kushuka daraja.
 
Back
Top Bottom