Iliishia nafasi ya pili mara zote mbili, msimu wa 1999-2000 na 2000-01. Ubingwa wa La Liga imenyakua mara sita katika historia yake. Kitu cha ziada kwake ni kunyakua ubingwa wa Copa del Rey mara saba. Valencia imecheza mechi 2,730 kwenye La Liga, ikishinda 1,217 na hivyo kukusanya pointi 4,290 kwa ujumla wake. Kwenye miaka ya 2000, Valencia ilikuwa moja kati ya klabu moto kabisa kwenye La Liga, ikitamba katika ligi ya ndani na kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.