Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maisha ya Pogba huko Old Trafford yamekuwa kwenye utata mkubwa tangu kikosi hicho kilipokuwa chini ya Jose Mourinho ambapo wawili hao walikuwa wakitibuana mara kwa mara. Baada ya ujio wa Ole Gunnar mambo yamebadilika, lakini kauli yake ya hivi karibuni ya kwenda kujiunga na Real Madrid ni ndoto yake imeanza kuzua utata mpya.
 
Wakati Man United ikitangaza hilo, wakala wa Pogba, Mino Raiola ameitaka Real Madrid kumfanya mteja wake kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi huko Bernabeu kama kweli inahitaji saini yake.
 
Tuttosport inaripoti Pogba anahitaji mshahara wa Euro 16 milioni kwa mwaka kama Real Madrid itamsajili au timu nyingine yoyote ile ikiwamo Juventus inayotajwa inahitaji huduma yake. Pogba ni mmoja kati ya majina kadhaa ya mastaa wanaosakwa na Real Madrid baada ya Kocha Zinedine Zidane kurudi kwenye timu hiyo na kupanga kuijenga upya.
 
Back
Top Bottom