Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Emery amepania kukifumua kikosi cha Arsenal katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto huku akisaka mlinzi wa kushoto, beki wa kati na kiungo mshambuliaji lakini yote haya yanategemea kama ataondoa baadhi ya mastaa.
 
Ozil amekuwa hana nafasi kubwa tangu ujio wa Emery na mshahara wake wa Pauni 350,000 kwa wiki umekuwa ukiitesa klabu hiyo, wakati huo huo Mkhitaryan amekuwa na kiwango cha kusuasua klabuni hapo tangu atue kutoka Manchester United Januari mwaka jana.
 
Kutokana na hilo, hizi hapa klabu sita zilizokusanya pointi nyingi zaidi kwenye mikikimikiki ya La Liga na kudhihirisha wazi ubabe wa Real Madrid na Barcelona kwenye michuano hiyo huku kumiliki mastaa wa maana katika vikosi hivyo kama vile Lionel Messi kwa Barcelona na Gareth Bale kwa Los Blancos wakizipa faida zaidi klabu hiyo katika kutamba kwenye La Liga.
 
6. Sevilla - pointi 3,602

Sevilla imefurahia kubeba mataji kadhaa kwenye michuano ya Ulaya kwa kuanzia mwaka 2006, ambapo klabu hiyo imebeba Europa League mara tano na kuongezea Copa del Rey mara mbili. Kuhusu La Liga haijabeba taji hilo tangu msimu wa 1945-46.
 
Sevilla inashika nafasi ya sita katika timu zilizokusanya pointi nyingi katika historia ya La Liga, ikicheza jumla ya mechi 2,474 ikishinda mechi 1,019, sare 545 na imekumbana na kipigo mara 910, hivyo kuifanya iwe imekusanya pointi 3,602 katika La Liga.
 
Iliishia nafasi ya pili mara zote mbili, msimu wa 1999-2000 na 2000-01. Ubingwa wa La Liga imenyakua mara sita katika historia yake. Kitu cha ziada kwake ni kunyakua ubingwa wa Copa del Rey mara saba. Valencia imecheza mechi 2,730 kwenye La Liga, ikishinda 1,217 na hivyo kukusanya pointi 4,290 kwa ujumla wake. Kwenye miaka ya 2000, Valencia ilikuwa moja kati ya klabu moto kabisa kwenye La Liga, ikitamba katika ligi ya ndani na kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
4. Athletic Bilbao - pointi 4,340

Bilbao ni moja kati ya klabu tatu ambazo hazijawahi kushuka daraja kutoka kwenye La Liga. Athletic Bilbao imebeba ubingwa huo wa Ligi ya Hispania mara nane huku mara yake ya mwisho kunyakua taji hilo ilikuwa msimu wa 1983-84. Kwenye La Liga, imecheza jumla ya mechi 2,828, ikishinda 1,227, sare 659 na kupoteza mara 942 na kuifanya kukusanya jumla ya pointi 4,340 zinazowafanya washike nafasi ya nne katika orodha ya timu zilizokusanya pointi nyingi kwenye historia ya La Liga. Bilbao ni moja kati ya timu bora kabisa kwenye ligi hiyo kutokana na kuzalishaa mastaa wa maana sana.
 
3. Atletico Madrid - pointi 4,456

Kwenye nafasi ya tatu ya orodha ya timu iliyovuna pointi nyingi kwenye historia ya La Liga ipo Atletico Madrid. Klabu hiyo ilibeba ubingwa wa La Liga mwaka 2014 na kutajwa hayo ni mafanikio yake makubwa kwa sababu imefanya hivyo wakati klabu nyingine za Real Madrid na Barcelona zikiwa kwenye ubora wao. Kwa muda mrefu Barcelona na Real Madrid zenyewe ndizo zilizokuwa zikichuana kuwania ubingwa huo kabla ya Atletico Madrid kufanya mambo na kubeba taji mbele ya wababe hao. Atletico Madrid imecheza mechi 2,680, imeshinda 1,280, kufungwa 784 na imevuna pointi 4,456.
 
2. Barca - pointi 5,462

Klabu bora kabisa ya Hispania katika karne hii. Barcelona imeshinda mataji manane ya La Liga tangu mwaka 2005 na msimu huu ipo kwenye wakati mzuri wa kunyakua taji lake la tisa la ligi hiyo. Kwenye rekodi zake za La Liga, historia, Barcelona imekusanya pointi 5,462 kutoka katika mechi zake 2,828 ilizocheza kwenye ligi hiyo. Mwendo wake unaoifanya iwe imebakiza pointi chache sana kuifikia Real Madrid ambayo ndiyo klabu iliyovuna pointi nyingi kwenye La Liga. Ikiongozwa na Messi ikitamba katika Copa del Rey.
 
1. Real Madrid - pointi 5,623

Wababe hawa wa Bernabeu maarufu kwa jina la Los Blancos wamebeba mataji ya La Liga mara 33. Bado wanaoongoza kwa kubeba ubingwa mara nyingi licha ya kushinda taji hilo mara sita tu katika miaka 20 ya karibuni. Real Madrid inashikilia rekodi pia huko kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikibeba taji hilo mara 13. La Liga imecheza mechi 2,828 imeshinda 1,686, sare 565 na imepoteza 577, hivyo imekusanya pointi 5,623.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…