Straika, Diego Costa alitoka uwanjani baada ya dakika 29 tu, akionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kumtolea lugha chafu, mwamuzi Gil Manzano na mwisho wa mchezo, Atletico Madrid walitoka patupu, wakichapwa 2-0 na ndoto zao kufifia kwenye kuusaka ubingwa wa La Liga msimu huu.
Hata hivyo, hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Atletico Madrid kumaliza mechi yao waliyokwenda kucheza Nou Camp wakiwa pungufu kiasi cha kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kuhisi wamekuwa wakionewa wanapokwenda kucheza uwanjani hapo.
“Ni kitu ambacho siku zote kimekuwa kikitokea Camp Nou,” alisema Koke.
Walimtoa nje Fernando Torres hapa, walimtoa Torres, nembo kubwa kabisa,” alisema Simeone na kuongeza. “Tangu wakati huo, basi yeyote anaweza kutolewa kwa kadi nyekundu kwa upande wetu.”
Felipe Luis, Arda Turan na Oscar Ortega - Supercopa de Espana, 2013
Felipe Luis alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 80, Turan alionyeshwa kadi nyekundu dakika 17 tu baada ya kuingia na kocha wa kikosi hicho, Ortega alionyeshwa kadi nyekundu na kuambiwa akakae jukwaani. Matokeo ya mchezo huo, Supercopa ilibebwa na Barcelona shukrani kwa kanuni ya bao la ugenini.
Kadi mbili za njano ndani ya dakika sita zilimfanya supastaa wa Atletico, Torres kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Nou Camp. Mabao mawili ya Luis Suarez yalitosha kuisaidia Barcelona kushinda mechi hiyo, licha ya kwamba Atletico walisonga mbele baada ya ushindi wao wa 2-0 kwenye mechi ya marudiano uwanjani Vicente Calderon.
Rafu mbaya dhidi ya Lionel Lessi ilimfanya beki wa pembeni wa Atletico Madrid, Felipe Luis kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 44 tu ya mchezo, kabla ya beki wa kati, Diego Godin kwenda kuungana na mwenzake huko nyumbani baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu iliyotokana na kadi mbili za njano. Barcelona ilishinda mechi hiyo kwa mabao ya 2-1.
Ilikuwa nusu fainali ya Kombe la Mfalme, wakati Atletico Madrid walipokwenda kuwakabili Barca katika uwanja wa Nou Camp. Mechi hiyo ilimshuhudia Carrasco akitolewa nje katika dakika 69.
OLE wako upite mbele ya mashabiki wa Arsenal kisha utaje jina la Phil Jagielka, shauri yako watakukimbiza.
Unajua kwa nini, beki huyo wa kati wa Everton, juzi Jumapili aliwapiga bao pekee na kuwaweka Arsenal kwenye wakati mgumu katika vita yao ya kuwania Top Four baada ya kipigo cha 1-0 huko Goodison Park.
Ni kama Wamasai, wao wanadhani ng’ombe wote duniani ni wa kwao! Hata akiwa nao elfu, bado atavizia zizi la Mnyantuzu ili aibe hao Kumi waliomo zizini! [emoji1][emoji1][emoji1]
Jagielka unaambiwa hata uhakika wa kucheza mechi hiyo haukuwepo, alilazimika kutumiwa na Kocha Marco Silva baada ya beki wa kati Michael Keane kuugua dakika za mwisho mwisho kabla ya mechi kuanza.
Bao moja la beki huyo limewaweka Arsenal kwenye presha kubwa na sasa kwenye ile Top Four, wanaweza kushushwa hadi kwenye namba tano huko kama Chelsea itakuwa imeshinda mechi yake ya usiku wa Jumatatu dhidi ya West Ham United.
Beki wa Chelsea, Gary Cahill msimu huu amekuwa akipambana na hali yake kupata nafasi ya kucheza tangu kocha Maurizio Sarri alipotua huko Stamford Bridge. Hata hivyo, kukosa nafasi ya kucheza hakujawahi kumtia shida sana kwa sababu amekuwa na rekodi nzuri za kushinda mataji ya kutosha akiwa na jezi cha Chelsea. Rekodi zake zinaonyesha Cahill amefunga mabao 27 katika Ligi Kuu England. Mabao 13 alifunga alipokuwa na kikosi cha Bolton, moja na Aston Villa na mengine 13 amefunga akiwa na The Blues.
Gwiji wa Leeds United, beki wa kushoto Ian Harte alikuwa matata kabisa kwenye Ligi Kuu England kwa kufunga mabao ya mbali pamoja na kuweka mipira kwenye nyavu kwa mipira ya friikiki.
Rekodi zake kwenye Ligi Kuu England, zinaonyesha kwamba staa huyo wa zamani wa Jamhuri ya Ireland amefunga mabao 28 katika kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi hicho cha Leeds kati ya mwaka 1995 na 2004. Harte alicheza pia kwenye vikosi vya Reading na Sunderland, huku mara ya mwisho alikuwa kwenye kikosi cha Bournemouth.