Hata hivyo…ni mhimu kuelewa kuwa kolesto katika mlo huwa si lazima ipandishe kolesto ya kwenye damu.
Kwa kawaida Ini peke yake huzalisha kiasi kingi cha kolesto kila siku. Wakati tunapokuwa tumekula mayai zaidi, Ini lenyewe huzalisha kiasi kidogo zaidi cha kolesto ili kusawazisha hiyo tofauti.
Mayai huuongeza Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto ijulikanayo kwa kiingereza kama ‘High Density Lipoprotein’ (HDL). Ambayo hujulikana kama ni kolesto nzuri, maana kuna kolesto nzuri na kolesto mbaya.
Watu wenye msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto kwa kawaida huwa na uwezekano mdogo wa kupatwa na maradhi kama ugonjwa wa moyo, stroke na matatizo mengine mengi ya kiafya.
Ndiyo, ni kiinilishe mhimu zaidi na mara nyingi hupangwa pamoja na vitamin za kundi B.
Hiki ni kiinilishe kinachopatikana katika mayai ambacho kazi yake kuu mwilini ni kutengeneza ukuta wa seli na kinacho kazi pia ya kutengeneza molekuli za hisia katika ubongo na kazi zingine nyingi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.