1. John Terry- mabao 41
Gwiji wa Chelsea, John Terry anashikilia rekodi ya kuwa beki aliyefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu England. Beki huyo amefunga mabao 41 katika mechi 492 za ligi alizoichezea Chelsea kuanzia mwaka 1998 hadi 2017. Katika michuano yote, amefunga mabao 67 katika mechi 717. Terry amekuwa na rekodi tamu kabisa kwenye kikosi hicho cha The Blues akishinda mara tano ubingwa wa Ligi Kuu, mara tano Kombe la FA, mara tatu Kombe la Ligi, mara moja Ligi ya Mabingwa Ulaya na mara moja nyingine Europa League. Kwa sasa ni kocha msaidizi huko Aston Villa.