Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sote tunapenda kuwa warembo, beautiful skin, nice hair (long or short), nails nakadhalika na hii hutupelekea kuwa tuntafuta bidhaa ambazo zitatufanya tuonekano warembo lakini kuna baadhi ya mamabo ambayo huwa tunasahau kwamba yapo na yanaweza kutuletea madhara
 
Bidhaa za urembo hu expire

Hili ni jambo ambalo inawezekana unalijua lakini hailifuatilii sana.Wengi tukinunua vipodozi tunapaka mpaka siku kitakapoisha bila kujali kama huo ni muda sahihi wa kukaa na kipodozi au lah! Kwa baadhi ya vipodozi kuna alama kama iliyozungushiwa kwenye picha.
 
Sponge aina zote ( mwezi 1-2)
Lotion aina zote (mwaka 1)
Shampoo na bidhaa za kustyle nywele (miaka 2)
Cream za kunyolea (miaka 2)
Deodorant,sabuni,mouthwash (miaka 3)
Mascara na wanja wa maji (miezi 3)
Foundation na concealer za maji (Mwaka 1)
Make up kavu za powder,Lipstick,lipgloss,wanja mkavu (Miaka 3)
 
Sponge aina zote ( mwezi 1-2)
Lotion aina zote (mwaka 1)
Shampoo na bidhaa za kustyle nywele (miaka 2)
Cream za kunyolea (miaka 2)
Deodorant,sabuni,mouthwash (miaka 3)
Mascara na wanja wa maji (miezi 3)
Foundation na concealer za maji (Mwaka 1)
Make up kavu za powder,Lipstick,lipgloss,wanja mkavu (Miaka 3)
 
Kuna bidhaa za ngozi zinazobadili umbo na muonekano

Kila unachopaka kwenye ngozi yako huathiri mwili wako kwa namna moja au nyingine kama ilivyo kwa vitu unavyokula na kunywa. Vitu unavyopaka hupenya ndani ya mwili wako na mabaki,uchafu,sumu huchujwa kwenye ini.
 
Baadhi ya bidhaa za urembo hubadili mfumo wa mwili hata kusababisha mtu aongezee uzito, atunze mafuta kiunoni na tumboni zaidi na hata kuotesha ndevu kwa mwanamke.Vipodozi vyenye corticosteroids (moja ya ingredients katika dawa za ngozi) ni moja ya vitu vinavyoweza kuleta madhara hayo
 
Corticosteroid huwekwa kwenye dawa za ngozi na hushauriwa kutumika si zaidi ya wiki mbili lakini uwezo wa baadhi ya corticosteroid kubadili rangi ya ngozi umefanya dawa hizi zitumike kwa muda mrefu sana tena kama lotion za kila siku na baadhi ya watengenezaji wa bidhaa za urembo pia huziweka katika bidhaa zao kinyume na sheria.
 
Corticosteroid zipo aina nyingi na baadhi ni clobetastole na betamethasome. Mfano wa lotion zenye Corticosteroid ni lotion maarufu ya CLONOVATE. Pia ingredients kama trichosan na phthalates huharibu balance ya hormone hivyo kuchangia katika kufanya mwili unenepe hovyo.Unaponunua bidhaa ni kuhimu kuchunguza vitu vilivyomo.
 
Natural/asili haimaanishi sahihi na isiyo na madhara.

Kumekuwa na muamko wa matumizi ya bidhaa asili sana. Kiujumla vitu asili ni bora zaidi kuliko vitu vinavyotengenezwa kiwandani na kuwekewa kemikali nyingi.
 
Pamoja na hilo kumbuka si kila kilichoandikwa asili basi ni asili kweli hivyo nunua kutoka kwa mtu anayeaminika. Pia kuna vitu ambavyo vina bidhaa asili au ni asili lakini vinaweza visiendane na ngozi yako au mwili wako kiujumla. Baadhi husababisha hata madhara ya allergy.
 
Pia kuna michanganyiko ya vitu asili ambayo si salama kwa ngozi yako na mwili mfano mitishamba inayopunguxa mwili kwa kuharisha, scrub za sukari au chumvi yenye vipande vikubwa kwa ngozi ya usoni (husababisha vichubuko midogo/micro tear).
 
Back
Top Bottom