Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MKATABA wa kiungo wa Manchester United, Ander Herrera, (29), unamalizika mwisho wa msimu huu, lakini mazungumzo ya kuongeza mkataba wake yanaonekana kutozaa matunda mpaka kufikia sasa.
 
Hata hivyo, wakati mwenyewe moyo wake ukiwa bado Old Trafford, Paris Saint-Germain wanasali kuhakikisha anatua kikosini mwao. Huku kwa kocha wake Ole Gunnar Solskjaer ni presha katika kuhakikisha anambakiza nyota huyo OT.
 
Huko uwanjani kazi yake inaonekana wazi. Wakati Paul Pogba na Nemanja Matic wakiwa bize kusukuma mashambulizi, nyuma yao pamekuwa na mtu makini wa kukaba. Mtu mwenye uwezo wa kutembea na kivuli cha viungo wa timu pinzani. Ndio huyu Herreira. Eden Hazard na Kylian Mbappe wanamjua vizuri.
 
Kwa upande wake, Andreas Perreira, kwa sasa hawezi kulaumiwa kwani amecheza dakika 389 tu, lakini ametoa asisti moja na kufunga bao moja, katika ushindi wa 3-2, walioupata dhidi ya Southampton.
 
WASTANI MZURI WA USHINDI

Katika mechi 19, ambazo Herrera ameingia dimbani na jezi ya United, mashetani wekundu wamepata ushindi mara 12 na kupoteza michezo mitatu huku sare zikiwa nne. Hii ni sawa na asilimia 63 ya ushindi.
 
JUKUMU LA KUKABA

Kama kitu kinachomtambulisha Herrera vizuri, ni uwezo wake wa kukaba.

Mhispania huyu anakaba hadi kivuli, ni mbishi balaa.

Eden Hazard, analijua hili. Takwimu zinaonesha kuwa, Herreira anaongoza kwa wastani wa kupokonya mipira na kuzuia mashambulizi.
 
Herrera ana wastani wa 2.4 wa kuzuia na wastani wa1.9 wa kupokonya mipira, ndani ya dakika 90, huku Fellaini akiwa na wastani wa 1.5 kuzuia na 0.3 wa kupokonya mipira.

Fred ana wastani wa 1.8 kuzuia mashambulizi na wastani wa 1.0 wa kupokonya mipira, kwa upande wake, Perreira ana wastani wa 0.7 wa kuzuia na 0.9 wa kupokonya mipira.
 
FUNDI WA PASI

Eneo lingine ambalo Herrera anawazidi wenzake ni uwezo wa kupiga pasi. Takwimu zinaonesha miguu ya Mhispania huyu, ndio inayoendesha kiungo ya United. Ana wastani wa 43.7 wa kupiga pasi katika kila mechi. Fellaini ana wastani wa 30.4, na Perreira (26.1). mtu pekee anayemkaribia ni Fred, mwenye wastani wa 43.5. sio hilo tu, lakini Herrera ni makini sana katika pasi zake. Ni fundi wa kupiga pasi za mwisho.
 
Anaongoza kwa kupiga pasi za mwisho.

Wastani wake wa kupiga pasi za uhakika, ni asilimia 88.2. Fred anafuatia kwa wastani wa asilimia 87.6, Fellaini (81.2%) na Perreira (85.1%).

Kwenye kikosi kizima cha mashetani wekundu, ni mabeki Victor Lindelof (88.8%) na Phil Jones (93.4%) , pekee ndio wanaomzidi Mhispania huyu, anayeendesha roho ya kiungo ya United kwa sasa.
 
Back
Top Bottom