Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati huo klabu kadhaa zilipewa ofa ya kumchukua lakini zilimkatalia. Klabu kama Corinthians, Palmeiras na Santos zote zilimtolea nje. Baadaye akaenda Ulaya katika nchi ya Ureno akijiunga na klabu ya Braga ambapo alianza kuonyesha makali yake kabla ya kuelekea Hispania.
 
Aliwahi kuwa katika shule ya soka ya Arsenal kabla ya kuachwa kwa kile kilichodaiwa kwamba alikuwa mdogo na anacheza taratibu. Mwaka 2015 kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kwamba lilikuwa kosa kubwa kumuona Kane akiondoka katika mikono yao.
 
Ronaldinho-St Mirren

Unachokiona kipo sahihi kabisa. Nusura staa huyu wa zamani wa Brazil aliyeinyanysa dunia kwa soka lake maridhawa ajiunge kwa timu vibonde ya Scotland St Mirren. Mwaka 2001 staa huyu tayari alikuwa na dili la kujiunga na PSG akitokea klabu ya Gremio ya kwao Brazil.
 
Hata hivyo ilihitajika aende katika timu fulani ya Ulaya kwa ajili ya kuanza kuzoea maisha ya Ulaya. Kocha wa wakati huo wa St Mirren, Tom Hendrie anadai kwamba kila kitu kilikuwa kimekwenda sawa na dili lilikuwa linakaribia kukamilika lakini klabu ya Gremio ikakwamisha dakika za mwisho kwa sababu za kisheria.
 
Historia ingeweza kuwa tofauti kwake kama klabu ya Independiente ya kwao Argentina ingemkubali akiwa mdogo. Inadaiwa kwamba waliwahi kugoma kumchukua kwa madai kwamba hakuwa na nguvu za kutosha kufanikiwa katika soka. Inter Milan wakatumia fursa hiyo.
 
Yaya Toure-Arsenal

Dhahabu nyingine iliyotoweka katika mikono ya Arsenal kimasikhara tu. Yaya alikwenda pale kufanya majaribio wakati huo kaka yake Kolo akiwa staa katika timu. Alicheza hadi mechi ya kirafiki kwa ajili ya kumshawishi Arsene Wenger amchukue.
 
Hata hivyo alishindwa kumfurahisha kocha huyo ambaye alida kuwa ‘Yaya alikuwa wa kawaida sana’. Wakasingizia kwamba Pasipoti yake na vibali vya kazi vingekuwa tatizo kwao. Yaya akaamua kuchukua njia tofauti na baadaye akaibuka kuwa staa mkubwa katika klabu za Barcelona na Manchester City.
 
Back
Top Bottom