Na hakuna madhara yoyote katika matumizi ya kukumanga bali uboresho wa urembo wa macho na ongezeko la mshawasha mzuri katika mwili katika mengi yenye uhitaji wa faragha.
Maharagwe imekuwa ni nafaka inayoliwa na watanzania tulio wengi hasa kutokana na kipato chetu. Lakini leo nataka nikwambia faida ipatiakanayo kwa matumizi ya nafaka hii katika afya mwanadamu.
Hakika si wengi tuliokuwa tunaijua siri hii, ndio maana nimeona haja ya kushirikiana na nyinyi katika Makala hii ndogo inayohusu maharagwe. Najua tulio wengi tunayajua maharagwe na makundi yake kadhaa.
Tafiti mbalimbali zimefanywa na wataalam wa maswala ya sayansi ya lishe na kupata majibu kadhaa ambayo leo nataka na wewe msomaji wangu upate kuyafahamu ili kama hupendelei kula maharagwe basi uanze mara moja pindi tu utakapomaliza kusoma Makala hii. Zifuatazo ni faida zipatikanazo kwa kula maharagwe;
Katika uchunguzi wa hivi karibuni wa jarida la American Collage of Nutrition umebaini kuwa watu wanaokula maharagwe wana 22% ya kupunguza uzito wa mwili. Na wana uwezekano mkubwa wa kuwa na viuno vidogo kuliko watu wasiokula kabisa maharagwe. Maharagwe yana kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi zinazozoyeyuka, ambazo zinapunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula na kukufanya kutosikia njaa kwa muda mrefu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.