Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Upendeleo wa kuamini, hapa unakubaliana na kitu kwa sababu tu unaamini hivyo. Imani yako inakufanya uone kwamba kitu hicho ni sahihi. Tunachopaswa kuelewa ni kwamba kama unaanza na kuamini, kila kinachoendana na imani yako kitakuwa sahihi.
 
Upendeleo wa mwonekano, huwa tunadanganywa na mwonekano wa nje, pale ambapo mtu au kitu kinaonekana kizuri kwa nje, tunaamini ni sahihi. Tunapaswa kujua kwamba hakuna kitu kinachodanganya kama mwonekano wa nje, na kama tunataka kuupata ukweli basi tuchimbe ndani zaidi.
 
Upendeleo wa kundi, kama kile ambacho tunataka kufanya kuna wengine wanafanya, huwa tunaamini ni sahihi, hata kama siyo. Waswahili wanasema kifo cha wengi ni harusi, au penye wengi hapaharibiki jambo, lakini siyo sahihi. Mara nyingi kinachofanywa na wengi huwa siyo sahihi.
 
Upendeleo wa kulaumu, wakati mwingine tunafanya maamuzi kwa ajili ya kuwalaumu wengine. Tunajiona kama wanyonge ambao hatuna kitu cha kufanya kwa kuwa wengine wametuzuia au kutukwamisha kwenye kile ambacho tunataka kufanya. Tunapaswa kujua kwamba hakuna tunayeweza kumlaumu kuhusu maisha yetu ila sisi wenyewe.
 
Upendeleo wa ubora, inapofika kwenye kufanya maamuzi, huwa tunaamini sisi ni bora kuliko wengine, tunajiambia sisi ni wasafi kuliko wengine na ni tofauti na wengine. Hivyo tunaamini kwa ubora wetu na usafi wetu, hatuwezi kufanya makosa ambayo wengine wanafanya, na hilo linapelekea kurudia makosa ambayo wengine wamekuwa wanafanya. Lazima tujue udhaifu wetu uko wapi na kuukabili ili tuweze kufanya maamuzi bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…