Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huu utafiti huu haumhusu Rolo Modo wangu. Watafiti wamechemsha [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
07873d349e7c8cbde217b11c6a7431db.jpeg
 
Barcelona – mataji 8, misimu 11

Katika misimu 11 ya mwisho, Barcelona wakiwa na huduma bora kabisa ya supastaa Lionel Messi, imebeba ubingwa wa La Liga mara nane. Mara nyingine tatu ilizokosa, mara mbili walibeba Real Madrid na mara moja Atletico Madrid.
 
Bayern Munich – mataji 10, misimu 14

Taji jingine la Bundesliga lipo njiani msimu huu kwa wababe Bayern Munich. Wababe hao wa Bundesliga wamekuwa wakiwashinda wapinzani wao huko kwa kuwa na uchumi mzuri kwa maana ya kuwa na uwezo wa kusajili wachezaji nyota kutoka kwenye timu wapinzani wao kama vile Borussia Dortmund. Dortmund walijaribu kufurukuta kimtindo, lakini Bayern ilienda kuwamaliza kwa kuwachukulia wachezaji wake nyota na hivyo wao kuendelea kutamba.
 
Juventus – mataji 8, misimu 8

Kwenye Serie A, Juventus imefanya ligi hiyo isiwe na maana kutokana na kubeba wao tu katika kipindi cha misimu minane mfululizo. Baada ya AC Milan na Inter Milan kuporomoka kwenye utawala wao, Juventus waliibukia na kuwa watawala kwenye ligi hiyo ya Italia.
 
AS Roma na Napoli zimekuwa zikifurukuta kwa siku za karibuni, lakini wamekuwa hawana uwezo wa kupambana na Juventus ambao wao kila msimu wanafanya usajili mpya wa kuboresha kikosi chake kama walivyofanya mwaka jana walipombeba supastaa Cristiano Ronaldo.
 
PSG – mataji 6,misimu 7

Pesa inaongea. Baada ya kuwa chini ya umiliki wa matajiri wa Qatar, Paris Saint-Germain imekuwa kwenye kipindi kizuri ikifanya usajili wa wachezaji inawataka na kutamba kwenye Ligi ya Ufaransa wakibeba ubingwa kama wanavyotaka
 
Kikosi chao kimepita nyota wengi kama vile Zlatan Ibrahimovich na sasa wana wachezaji mahiri kama Kylian Mbappe na Mbrazili, Neymar. Katika misimu saba iliyopita, PSG imebeba ubingwa mara sita na kushindwa mara moja tu, ambapo AS Monaco ilipambana na kunyakua ubingwa huo. Lakini, baada ya Monaco kuonekana kuwa tishio, PSG ilivamia hapo kusajili nyota matata.
 
Kwenye Ligi Kuu England mambo ni tofauti kabisa hakuna bingwa wa kudumu. Kwa msimu huu mapambano yamekuwa makubwa, Man City wakichuana na Liverpool na yeyote anayweza kubeba taji hilo. Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, kuna mabingwa watano tofauti, Man City, Chelsea, Man United, Arsenal na Leicester City wote wamebeba taji hilo la ubingwa wa ligi.
 
Back
Top Bottom