Kwenye Ligi Kuu England mambo ni tofauti kabisa hakuna bingwa wa kudumu. Kwa msimu huu mapambano yamekuwa makubwa, Man City wakichuana na Liverpool na yeyote anayweza kubeba taji hilo. Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, kuna mabingwa watano tofauti, Man City, Chelsea, Man United, Arsenal na Leicester City wote wamebeba taji hilo la ubingwa wa ligi.