FARAJA YA UAMINIFU
SIKU moja, watoto wawili; mvulana na msichana, walikuwa wakicheza pamoja. Mvulana alikuwa na gololi nyingi za marumaru ilhali msichana akiwa na peremende za maziwa kwenye mfuko.
Kama zilivyo tabia za watoto, kila mmoja akatamani cha mwenziye. Mvulana akapendekeza wabadilishane. Msichana akaafiki na kukabidhi peremende zote. Na mvulana naye akakabidhi gololi zake, lakini kisirisiri akafanikiwa kuificha gololi moja kubwa na nzuri.
Siku hiyo, msichana alilala kwa amani akifurahia gololi alizojipatia. Lakini mvulana hakupata usingizi kwa hofu kwamba, huenda msichana alimuingiza mkenge kwa kuficha peremende nyingine tamu zaidi - kama ambavyo yeye alificha gololi kubwa.
FUNZO: Kama hutojitoa kwa asilimia mia moja kwenye mahusiano (au jambo lolote), siku zote utateketea moyoni ukidhani na mwenziyo anaficha baadhi ya asilimia zake sehemu nyingine.