Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FARAJA YA UAMINIFU

SIKU moja, watoto wawili; mvulana na msichana, walikuwa wakicheza pamoja. Mvulana alikuwa na gololi nyingi za marumaru ilhali msichana akiwa na peremende za maziwa kwenye mfuko.

Kama zilivyo tabia za watoto, kila mmoja akatamani cha mwenziye. Mvulana akapendekeza wabadilishane. Msichana akaafiki na kukabidhi peremende zote. Na mvulana naye akakabidhi gololi zake, lakini kisirisiri akafanikiwa kuificha gololi moja kubwa na nzuri.

Siku hiyo, msichana alilala kwa amani akifurahia gololi alizojipatia. Lakini mvulana hakupata usingizi kwa hofu kwamba, huenda msichana alimuingiza mkenge kwa kuficha peremende nyingine tamu zaidi - kama ambavyo yeye alificha gololi kubwa.

FUNZO: Kama hutojitoa kwa asilimia mia moja kwenye mahusiano (au jambo lolote), siku zote utateketea moyoni ukidhani na mwenziyo anaficha baadhi ya asilimia zake sehemu nyingine.
 
Mara nyingi, binti alikuwa akimfikia baba yake mzazi, kumshitakia adha anazopitia kwa mumewe. Ili kumtuliza ghadhabu bintiye, baba alimwambia jambo la kuchekesha; binti akaangua ucheko.

Baada ya dakika chache, baba alirudia tena kichekesho kilekile, binti akaishia kutabasamu tu. Baada ya sekunde kadhaa, baba alirudia tena kichekesho kilekile; binti hakucheka.

Sasa baba alitabasamu na kusema: "Najua huwezi kuchekeshwa muda wote kwa kichekesho kilekile. Sasa viweje wewe walizwa kila siku na tatizo lilelile?"

Fanya maamuzi: vumilia tatizo, au liondoe.
 
kwa hiyo ed woodward ndiye fala wa sokoni?

Madrid and Zidane made it clear that they can they want Bale to leave; the perfect scenario would have been Manchester United’s Ed Woodward turning up and paying more than he really should. That was hoped for, but Woodward hasn’t taken the bait, at least not yet.
 
Laurent Koscielny denounces the decision to hold Europa League final in Baku. “I think Uefa needs to know about the different problems they can have with the politics in the country. When one country has a problem with another they should not give the final to that country.“
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…