Afrika ni bara la pili kwa ukubwa pia ni bara la pili kwa kuwa na watu wengi. Afrika ina ukubwa wa kilometa za mraba 30,244,049 pamoja na idadi ya watu inayozidi 1,216,130,000.
Kisiwa kikubwa zaidi Afrika ni Madagascar, kinapatikana bahari ya Hindi na kina ukubwa wa kilometa za mraba 587,713. Pia kisiwa hiki ni cha nne duniani kwa ukubwa na cha pili kwa nchi kubwa ambazo ni visiwa.

Maporomoko ya maji ya Victoria yaliyoko mpakani mwa Zambia na Zimbabwe, ni moja ya maajabu ya dunia. Mto zambezi ni chanzo kikubwa cha maji ya maporomoko hayo.
Ziwa viktoria ni ziwa kubwa zaidi Afrika na la tatu duniani kwa ukubwa (Kilometa za mraba 69,485). Ziwa hili lipo eneo la maziwa makuu likihusisha Tanzania, Kenya na Uganda.
Afrika na Ulaya imetengwa na bahari kwa karibu zadi kwa kilometa 14.3 kati ya Hispania na Morocco. Inasemekana kuwa nchi hizi ziko kwenye mazungumzo ya kujenga daraja ili kuziunganisha na kurahisisha usafiri.