Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20190527-WA0015.jpeg
 
Taswira ya Lisu aliechezea risasi zilizolengwa kumuua kabisa na jinsi gani Mungu amezuia ashki ya mtu ya kutaka kumaliza uhai wa mwengine. Risasi zaidi ya thalathini lakini mwaka sasa na anaendelea vizuri tena akibeba ari ya “I’ll be back”. Unafikiri kajifunza nini katika huu mkosi uliomfika? Imani yake? Msimamo wake? Taifa linamtazamaje kwa sasa?
 
Halkadhalika itathmini nafsi ya mwanaadam iliopewa mdomo na pumzi ya kusema alitakalo kiasi ya kufika kilele cha ashki akalewa na sifa zake mwenyewe na kujitangaza ya kwamba anaweza kufufuliwa siku ya siku akiwa kiongozi wa malaika hasa, watiifu wasiobeba chochote zaidi ya haki na kile alichowaamrisha Mwenyezi Mungu.
 
Lakini mdomo huo huo wake mwenyewe, na walinzi waliomzunguka, na silaha walizobeba, ukamjibu kwa qadar ya Mwenyezi Mungu, akajitangaza yeye na waliomzunguka kuwa ni kichaa kabisa asieambilika tena hadhira ile ile ikipiga makofi ya kumtukuza. Yaani mwenye jeshi na amri ya juu anajiita chizi na washauri wake. Bila ya shaka hakutatokea malaika wakaongozwa na kichaa wa tafsiri yoyote ile maana si sifa inayosadifu ubora wa kiumbe.
 
Wanafunzi watakaoshika mimba hawana ruhusa ya kuendelea na elimu hata ikiwa ni haki yao kama binaadam na kama mwananchi wa nchi hii inayolinda haki ya elimu. Yaani kumkosesha elimu mwanafunzi mjauzito ni sawa pia na kutoa fursa ya kumkosesha huduma ya afya kwa sababu vyote hivi vinaendana kwa misingi ya haki kama ilivyo haki ya kuishi.
 
Lakini cha ajabu ni kwa aliehukumiwa kosa la ubakaji. Huyu si mtuhumiwa tena bali ni “Convict” tena katika ubakaji. Kweli kulikuwa na haja ya hii “glorification” ya mwenye hukumu ya ubakaji akafanywa hero? Au tuseme alionewa? Jee haki ya kuchafuliwa jina lake na kukaa ndani miaka yote italipwa na hii “gesture” ya kumpa msamaha wakati anatembea na kivuli cha hukumu ya ubakaji?

nimemkumbuka babu seya
 
Tazama namna ya umasikini kwa wenzetu unavyopigwa vita kivitendo badala ya akili mgando na kauli za rejareja. Wenzetu wana mfumo unaoitwa Tax credit, ambao umegewawia katika sehemu mbili. Moja ni kwa wenye watoto lakini wazazi au mzazi hana kazi. Na pili ni kwa wenye ajira lakini wakiwa na masaa kidogo na pato dogo lisilotosheleza.
 
Back
Top Bottom