Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

59893601_387102645227774_4724053399496189121_n.jpg
 
Hahahaha, pole Kiongozi
ni shidaa, banter kidogo
siku moja nilikuwa nimevalia full nguo zangu za msiba wa dini ya kikristo (nyeusi), si unajua tena sisi wengine tumerithi uchafu badaka ya kurithi utajiri.

mara paap nikapata offer ya kufanya mahojiano ya kuajiriwa kupitia ofisi fulani na mshara ilikuwa ni shilingi 500 kwa siku.
ebwana weee si nikapita barabarani nyakati za asubuhi, nilikutana na mvua ya kinyesi cha kunguru hatimaye nilijikuta nguo zote zikibadilika rangi kutoka black to white maziwa from kolomijee.

interview ikanishinda kwa sababu sikuwa na nguo nyengine,
 
Scholl nusura afunge bao kutoka hatua 20 baada ya kupokea pasi murua ya Basler lakini mpira huo ukagonga mwamba na kurudi katika mikono ya Schmeichel. Zikiwa zimebakia dakika 10, Ferguson aliamua kumuingiza Ole Gunnar Solskjær ambaye mara baada ya kuingia alimlazimisha Kahn kucheza vema mpira wake murua wa kichwa. Hiyo ilikuwa kosakosa ya hatari zaidi kwa United.
 
Dakika moja baadaye Bayern ilikosa nafasi ya kujihakikishia ushindi baada ya Jancker kujipindua hewani lakini mpira wake ukatoka nje kidogo ya mwamba. Dakika tano za mwisho, Teddy na Ole walimlazimisha Kahn kuokoa michomo miwili ya hatari. Kwanza kwa shuti la Teddy na kisha kwa kichwa cha Ole.
 
Kona ilipigwa na Dwight Yorke akauparaza mpira kwa kichwa huku Thorsten Fink akishindwa kuuosha vema. Mpira ukamfikia Ryan Giggs ambaye alijaribu kupiga kwa mguu wa kulia lakini shuti lake likawa la ovyo na mpira ukaenda kwa Sheringham, aliyeugusa tu kwa mguu wa kulia ukaingia wavuni. Bao hilo liliandikwa limefungwa dakika ya 90 na sekunde ya 36.
 
Carsten Jancker alipoteza fahamu. Matthaus ambaye baadaye alitolewa katika mechi hiyo zikiwa zimebakia dakika 10 pambano kumalizika alikuwa amepoteza fainali yake ya pili ya Ulaya katika mazingira hayo hayo. Mwaka 1987 alikuwepo katika kikosi cha Bayern Munich ambacho kilipoteza kwa mabao mawili ya dakika za mwisho kwa Porto.
 
Rais anaitwa Rais kwa sababu kuna watu, si kwa sababu kuna wanyama au kuna mafuta ardhini. Tukizinduka na kukubali hali hiyo ndipo,tutatoka katika hali ngumu ya kihistoria ambayo imeufanya ulimwengu uwe na mabwana na watwana, uwe na wamiliki na wamilikiwa, uwe na wenye amri na wa amriwa, uwe na wenye haki ya kuishi na haki ya kufa.
 
Back
Top Bottom