Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Bayern, Ottmar Hitzfeld alijibu mapigo kwa kumuingiza kiungo Mehmet Scholl, ambaye hapohapo alimuandalia mpira vema Stefan Effenberg aliyepiga shuti lililokwenda nje kidogo. Schmeichel akaendelea kuibeba United alipopangua vema shuti jingine la Effenberg dakika ya 75.
 
Hahahaha, pole Kiongozi
 
Scholl nusura afunge bao kutoka hatua 20 baada ya kupokea pasi murua ya Basler lakini mpira huo ukagonga mwamba na kurudi katika mikono ya Schmeichel. Zikiwa zimebakia dakika 10, Ferguson aliamua kumuingiza Ole Gunnar Solskjær ambaye mara baada ya kuingia alimlazimisha Kahn kucheza vema mpira wake murua wa kichwa. Hiyo ilikuwa kosakosa ya hatari zaidi kwa United.
 
Dakika moja baadaye Bayern ilikosa nafasi ya kujihakikishia ushindi baada ya Jancker kujipindua hewani lakini mpira wake ukatoka nje kidogo ya mwamba. Dakika tano za mwisho, Teddy na Ole walimlazimisha Kahn kuokoa michomo miwili ya hatari. Kwanza kwa shuti la Teddy na kisha kwa kichwa cha Ole.
 
Kona ilipigwa na Dwight Yorke akauparaza mpira kwa kichwa huku Thorsten Fink akishindwa kuuosha vema. Mpira ukamfikia Ryan Giggs ambaye alijaribu kupiga kwa mguu wa kulia lakini shuti lake likawa la ovyo na mpira ukaenda kwa Sheringham, aliyeugusa tu kwa mguu wa kulia ukaingia wavuni. Bao hilo liliandikwa limefungwa dakika ya 90 na sekunde ya 36.
 
Carsten Jancker alipoteza fahamu. Matthaus ambaye baadaye alitolewa katika mechi hiyo zikiwa zimebakia dakika 10 pambano kumalizika alikuwa amepoteza fainali yake ya pili ya Ulaya katika mazingira hayo hayo. Mwaka 1987 alikuwepo katika kikosi cha Bayern Munich ambacho kilipoteza kwa mabao mawili ya dakika za mwisho kwa Porto.
 
Rais anaitwa Rais kwa sababu kuna watu, si kwa sababu kuna wanyama au kuna mafuta ardhini. Tukizinduka na kukubali hali hiyo ndipo,tutatoka katika hali ngumu ya kihistoria ambayo imeufanya ulimwengu uwe na mabwana na watwana, uwe na wamiliki na wamilikiwa, uwe na wenye amri na wa amriwa, uwe na wenye haki ya kuishi na haki ya kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…