Mei 12 2012: Fainali ya Michuanio ya Kombe la Ujerumani - Borussia Dortmund 5-2 Bayern Munich, Olympic Stadium, Berlin
Ilianza vyema kwa Klopp.
Baada ya kushinda mataji mawili ya Bundesliga akiwa na Borussia Dortmund, aliishindia klabu hiyo taji la tatu la michuano ya kombe la Ujerumani baada ya kuirarua Bayern Munich mjini Berlin chini ya Jupp Heynckes.
Robert Lewandowski, ambaye baadae alihamia Bayern, alifunga hat-trick huku mabao mengine ya Dortmund yakifungwa na Shinji Kagawa, ambaye baadae alihamia Manchester United, na Mats Hummels, ambaye pia alijiunga na miamba wa Munich.