Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utajilaumu mwenyewe

Kujilaumu hakuepukiki katika safari ya mafanikio hasa pale unapokuwa umepata tatizo au hasara kwa uamuzi ulioufanya hapo awali. Kwa hakika, huwezi kubadili uamuzi au tendo lililopita; badili uelekeo wa maisha yako ya baadaye kuanzia ulipo. Usijilaumu tena kwani utauwa ile hamasa yako ya dani na hutoweza kufikia mafanikio yako.
 
Utaanguka

Kuanguka ni hatua inayowakabili watu wengi sana katika safari yao ya mafanikio. Tatizo ni namna watu wanavyoshughulikia kuanguka kwao, kumbuka β€œUsiulize umeangukia wapi bali uliza umejikwaa wapi”.
 
Kwa mfano inawezekana umekopa mkopo na umepata hasara katika biashara na kupoteza fedha nyingi, badala ya kuendelea kulalamika tafuta namna ya kuziba pengo hilo ili uweze kuendelea mbele. Kujifunza kutafuta tatizo na chanzo chake kutakuwezesha kuliepuka wakati mwingine mbeleni.
 
Nakukumbusha tena na tena kuwa safari ya mafanikio inahitaji jitihada nyingi na kutokata tamaa. Kumbuka kuwa wanaojaribu mchezo wa riadha na kuacha njiani hawapewi tuzo bali wanapewa wale walioshinda pekee. Jitahidi kufanya bidii bila kuruhusu kukata tamaa au kurudishwa nyuma na mtu au kitu chochote.
 
 
Hahahahahahahaha, naona umemtolea povu kiaina bro wako[emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…