Asante sana shemeji. Kama akina baba tuna jukumu kubwa mno kwa wanetu. Wanasaikolojia wanasema kuwa ni afadhali mtoto akataliwe/atendewe mabaya na mama kuliko baba. Akikataliwa/akitendewa mabaya na baba yake, madhara yake ni makubwa mno katika maisha yake. Tunalo jukumu takatifu la kuhakikisha kuwa tunaacha mifano myema na tunaendelea kuishi kupitia kwa wanetu hawa siku tukiondoka.
Kabinti kangu haka nimekazoesha breakfast in bed wakati wa birthday zote. Na kenyewe leo kamelipa fadhila. Kamenipikia na kuniletea kitandani scrambled eggs, chai, turkey bacon na orange juice. Pia nimepata kadi nzuri iliyosainiwa na marafiki wa kenyewe pamoja na vijisenti vichache hivi.
Mungu Aendelee kutupa maarifa na ufahamu ili tuendelee kutimiza jukumu la Mungu kwa wanetu hawa Aliotupa. Hili ndilo jukumu letu kuu kuliko yote hapa duniani kama akina baba [emoji1545][emoji1545][emoji1545]