Wakati wa michezo ya ligi kuu ya klabu hiyo, kwa mfano, mashabiki wamekuwa wakiimba wimbo uliotungwa na mwanamuziki wa Marekani mwenye asili ya Afrika katika miaka ya 1920, wa Kum Ba Ya (Come by Here), kwa maneno: “Sheikh Mansour m’lord, Sheikh Mansour, oh lord, Sheikh Mansour,” wakiwa na maana ya kumsifia Sheikh Mansour bin Zayed, mmiliki wa Manchester City ambaye pia ni Waziri wa Ofisi ya Rais katika UAE, na kaka yake wa mama tofauti, Rais wa UAE, Khalifa bin Zayed Al Nahyan.